Na Mwandishi wetu
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) imesema kuwa
kuwa asilimia 64 ya umeme unaotumika nchini unazalishwa kwa kutumia gesi asilia na manufaa ya gesi hiyo ni makubwa zaidi ya kuzalishia umeme.
Akizungumza Jana mara baada ya kutembelea banda la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Felchesmi Mramba katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Alisema tangu ugunduzi wa gesi umefanyika nchini matumizi ambayo yametumika ni kuzalisha umeme ambapo kwa sasa karibu asilimia 64 ya umeme wote unaotumika nchini unazalishwa kwa kutumia gesi hiyo asilia.
Mramba alisema umeme wa maji nao ni miongoni mwa chanzo kinachozalisha Umeme kwa kushika nafasi ya pili huku vyanzo vingine vidogo vinachangia kwa kiasi kidogo.
" Mazungumzo baina ya serikali kuhusu mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi asilia (LNG) yamefikia mwishoni na sasa tupo kwenye hatua zinazofuatia na kwamba manufaa yanayotarajiwa ni kuweza kuanza kunufaika na gesi ambayo imegunduliwa kwa muda mrefu na haijaweza kutumika kwa kiasi kikubwa,"alisema na kuongeza
Alisema mradi wa LNG ndio utakaowezsha gesi ya Tanzania kuuzwa nje ya nchi na kwamba zipo namna chache ya kutekeleza jambo ikiweno ya kutengeneza mabomba na kuisafirisha kwa njia hiyo kwenda nchi za karibu.
"Njia nyingine ni kuigandisha ili iwe katika hali ya kimiminika na hivyo inapakiwa kwenye meli kubwa na kupelekwa nchi za ngambo, huko ndipo kutatuletea fedha za kigeni, sasa tunapokuwa na miradi mikubwa kama hii tunapaswa kujiangaa kwani mradi wa LNG utaleta ajira na matumizi mengine ya gesi," alisisitiza
Aidha alisema wanajiandaa mapema mwakani kuanza kutangaza kutoa vitalu kwa wawekezaji mbalimbali wanaofanya utafiti wa kugundua gesi zaidi au mafuta.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...