Hatimaye baada ya safari ya mchana na usiku mwanadada mpiga kinubi, kifaa chenye heshima kubwa nchini Ireland, Siobhan Brady, leo Julai 25, 2023, ameweka rekodi ya Dunia ya Guiness juu ya Mlima Kilimanjaro, Tanzania.

Siobhan ambaye mwaka 2018 aliweka rekodi Mlima Himalaya, India futi 16,000, sasa leo ameitangaza Tanzania zaidi na Mlima wetu Kilimanjaro kwa kuweka rekodi iitwayo “Guiness World Record for the Highest Harpist Concert” kwenye kilele cha juu zaidi duniani futi 19,000 Uhuru Peak ambapo muda nfupi uliopita alifanikiwa kupiga kinubi kwa dakika 34 wakati ili kuvunja rekodi alitakiwa walau dakika zisizopungua 18 akichanganya nyimbo mbalimbali kutoka Ireland na mataifa mengine ya Ulaya.

Tukio hilo limerekodiwa na chombo kikubwa cha habari duniani The National Geographic. Sasa Kamati ya Dunia ya Guiness itakaa kuthibitisha rekodi hiyo.

Ameweza na ameweza tena. Hongera kwa wote waliofanikisha, hongera Watanzania. Hureeeeeee!!!!!



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...