CHUO Kikuu Mzumbe wawakaribisha katika banda lao kwenye maonesho ya biashara ya Kimataifa ya 47 ili kujifunza teknolojia na ubunifu walionao kwa mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo Juni 30, 2023 na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, anayesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam( DVC ARC) Dkt. Eliza Mwakasangula. Amesema licha ya teknolojia mpya walizanazo pia wanawakaribisha wananchi kwa ujumla kwenda kufanya udahili wanafunzi wapya kwa mwaka wa masomo wa 2023/2024.
"Tunawakaribisha tunahuduma mbalimbali, tunadahili wanafunzi kwaajili ya kujiunga na Program zetu Chuo Kikuu Mzumbe kwa ngazi ya Shahada za awali kwa wale waliomaliza kidato cha nne, kidato cha Sita na hata waliomaliza muda mrefu." Amewakaribisha wananchi
Pia amewakaribisha wanafunzi wa Mzumbe (Alumni) kuchangia ujenzi wa hoteli za Kike katika Kampasi ya Mbeya ambapo Kampeni yake imeshazinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homela, ..."Kwa waliosoma Mzumbe lazima warudishe kidogo, kuonesha kwamba wewe ni mwanajamii wa Chuo Kikuu Mzumbe, kwahiyo tunakaribusha watu wote ambao wanaweza kuchangia."
Licha ya kuwakaribisha pia amewaomba wananchi kwa ujumla kuchangia ujenzi wa hosteli za Wanachuo wa kike katika kampasi ya Mbeya kupitia control namba 994180331310.
Hakuishia hapo Dkt. Eliza amesema kuwa Mzumbe wapo Vizuri katika kutoa elimu ya Sayansi na Teknolojia, Sheria, Uhasibu, Utawala. Pia amesema katika maonesho hayo wanateknolojia mbalimbali zinazotatua matatizo katika jamii.
Ikumbukwe kuwa Chuo Kikuu Kinakampasi tatu ambazo ni Mororgoro(Makao Makuu), Mbeya na Dar es Salaam ikiwa na Kituo cha Tegeta wanapotoa shahada za awali.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam( DVC ARC) Dkt. Eliza Mwakasangula(kulia) akiangalia Moja wapo ya bidhaa zilizotengenezwa na Mercy Mwambe , Mwanafunzi wa Masomo ya Shahada ya Uongozi wa biashara katika Ujasiliamali na ubunifu, katika maonesho ya 47 ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Frank Msonge akitoa maelezo kuhusiana na kitanda ambacho kitakuwa na rekodi za mgonjwa hii itaepusha Madaktari kutokuchanga taarifa za mgonjwa hata atapohamishiwa kitanda kingine.
Picha ya pamoja.
Baadhi ya wananchi wakipata huduma katika banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika maonesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...