Njombe

Wajumbe wa kamati tendaji ya Chama cha walimu wilaya ya Ludewa mkoani Njombe (CWT) wameazimia kwa pamoja kuto ingia kwenye uchaguzi wa nafasi ya mjumbe wa kamati kuu tendaji Taifa kutoka mkoa wa Njombe baada ya kufutwa uanachama mjumbe wa nafasi hiyo Mwl Thobias Sanga na wengine 18 wakidai kuwa hawajaona makosa ambayo yangewaondolea uanachama wao wajumbe hao.

Mwenyekiti wa Chama cha walimu (CWT) wilaya ya Ludewa Said Nyingo amebainisha hayo wilayani humo wakati akizungumza na vyombo vya habari juu ya msimamo kutokana na migogoro ya viongozi wao ngazi ya Taifa inayoendelea.

"Kikao kiliisoma barua ya kaibu mkuu wa chama cha walimu Tanzania ikiarifu kuwa MAKUT 18 akiwemo KUT wa Njombe na baadhi ya viongozi wa kitaifa walifutiwa uananchama,wajumbe waliradidi vifungu na hawakuliona kosa lolote ambalo lingewaondolea uanachama wao zaidi ya hayo mchakato huo ulikiuka katiba toleo la 6 ya mwaka 2014 kwenye ile ibara ya 41.2"alisema Nyingo

Nyingo aliongeza kuwa "Tarehe 25,7,2023 katibu wa CWT mkoa wa Njombe alitoa tangazo la nafasi wazi ya mjumbe wa kamati tendaji taifa anayewakilisha mkoa wa Njombe,kamati tendaji wilaya ya Ludewa tunatoa tamko kuwa kamati haifurahishwi hata kidogo na mivutano ya viongozi wa kitaifa lakini mbili haikubaliani na mchakato uliotumika kuufuta uanachama KUT wa Njombe na MAKUT Wenzake na tatu kamati imeazimia haitashiriki katika uchaguzi wa KUT uliotangazwa na katibu wa Chama cha walimu mkoa wa Njombe

Chefas Mdesa ni mwakilishi wa walimu vijana wilaya ya Ludewa ametoa wito viongozi kuishi malengo ya uanzishwaji wa Chama hicho ili kurejesha imani ya waalimu kwa taasisi yao pendwa kwa kuwa endapo wakiingia kwenye uchaguzi tena wanaamini watakuwa bado wakiendelea kukiuka katiba huku Mwalimu Asifiwe Haule akiwataka viongozi kujua kuwa wamiriki wa Chama ni wanachama.

"Endapo tukiingia kwenye uchaguzi maana yake na sisi bado tutakuwa tunakiuka katiba sasa sisi tunachoomba tutembee kwenye katiba"amesema Mdesa

Kwa upande wao Ibrahim Mgaya Mwakilishi wa walimu shule ya sekondari Lugarawa pamoja na Agness Mwinuka Mwakilishi wa walimu wanawake wilaya ya Ludewa wamesema kuwa kuingia kwenye uchaguzi kwa sasa ni kuzidi kukiongezea gharama chama na kuwaomba viongozi wao kukaa na kujadili ii kumaliza migogoro yao na kutokuingizia hasara Chama kwa kuwa pia baadhi ya wanachama wameanza kukatishwa tamaa na mwenendo wa uendeshaji wa Chama.


Ikumbukwe sakata hilo ni muendelezo wa migogoro iliyopo ndani ya Chama hicho ambapo baadhi ya viongozi taifa akiwemo Rais wa Chama hicho Mwalimu Lea Ulaya pamoja na Katibu Mwalimu Japhet Maganga wamekuwa wakiendelea kutuhimwa kwa changamoto mbalimbali ikiwemo kushindwa kuongoza chama kwa kufanya uhamisho wa walimu usiofuata utaratibu,matumizi mabaya ya madaraka pamoja na matumizi mabaya ya fedha.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...