NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
DIRA ya Maendeleo ya Taifa 2025 imeweza kuzingatia masuala ya kijinsia ambapo mambo mengi yametekelezwa ka kuwapa fursa vijana wa kike na wakiume kujifunza na kuonesha uwezo wao kwenye masula ya kijamii na kiuchumi.
Akizungumza katika Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) Mtandao wa Jinisia Tanzania TGNP, Afisa Programu Sera TGNP, Bi.Leogate Leokake amesema kwenye Dira hiyo mambo mengi yametekelezwa ikiwemo mradi wa Kujenga Kesho Iliyobora ambapo Mradi huo umewapa fursa vijana kujifunza.
Aidha amesema kuwa Katika Dira ya Maendeleo tumeona shughuli zingine za nchi ikiwemo mikopo ya asilimia 10 pamoja na kushuhudia watoto wa kike kupata ujauzito kurudi shuleni ambapo ni hatua kubwa Dira hiyo imeweza kuzingatia masula ya kijinsia.
Amesema kupitia Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 wanatarajia kutoka na mapendekezo ya pamoja kama wananchi kwamba wanatamani mchakato uweje katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 katika uboreshaji kwenye meneo ambayo yanahitaji uboreshaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...