Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
KATIBU Mtenda wa Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo wa Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt.Adolf Rutayuga amesema kuwa wanafunzi wanahitimu katika vyuo vya ufundi wanatoka na kwenda kufanya kazi.
Dkt.Rutayuga ameyasema hayo katika banda la NACTVET kwenye maonesho ya 18 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa sifa kubwa ya wahitimu wa vyuo vya ufundi wakihitimu kwenda kufanya kazi ni kutokana na masomo yao ni vitendo zaidi kuliko kukaririshwa kwa nadharia.
Amesema kuwa dunia ya sasa inataka wanafunzi wanapokuwa katika vyuo kuangalia fursa zilizo na changamoto kwenda kutatua kutokana na ujuzi waliopata ambao vyuo vya ufundi vinatoa majibu ya wanafunzi kuwa sehemu ya kutatua changamoto zilizopo.
Dkt Rutayuga amewataka wananchi kutrmbelea banda la NACTVET kupata elimu kuhusia na vyuo vya ufundi.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu la Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt.Adolf Rutayuga akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa NACTVET kwenye Maonesho ya 18 ya Vyuo Vikuu yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...