Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
BAADA ya kumalizana na Al Ahly SC, Winga Luís José Miquissone amezua mijadala huko mitandaoni akihusishwa kurejea nchini Tanzania kwenye Klabu yake ya zamani ya Simba.

Miquissone na Al Ahly SC wamefika makubaliano ya pande zote mbili kuvunja mkataba. Winga huyo machachari anahusishwa kutua Simba SC na tetesi zimekuwa nyingi huku wengine wakiwa na uhakika wa asilimia 100% kuwa Miquissone amemalizana na mabosi wa Simba SC.

Kupitia chapisho lake kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo mtandao wa ‘Instagram’, Miquissone ameandika ujumbe kwa kimombo ulioenda sambamba na picha ya andiko la kuachana na Al Ahly. Miquissone amesema: ‘This is official is time to restart’ akimaanisha kuwa ni muda rasmi wa kuanza upya.

Baada ya chapisho hilo la Miquissone, Mwamba wa Lusaka, Clatous Chama hakuacha ujumbe huo upitie hivi hivi, Chama alijibu ujumbe huo kwenye ‘comments’ kwa kusema: ‘Twende mwanangu’. Hiyo ni ishara yaweza kuwa Miquissone atarudi tena nchini!

Hata hivyo, Rais wa Heshima wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (MO Dewji) ameendelea kuchapisha misemo inayohusiana na usajili wa wachezaji wapya Klabuni hapo. MO Dewji kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ameandika: “Kijana amemalizana na Klabu namba moja Afrika, haya sasa tuone anafanya nini?”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...