Na Mwandishi Wetu

MAONESHO ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam, yanayofanyika katika viwanja vya SabaSaba, yamekuwa ni fursa adhimu kwa wadau mbalimbali kushuhudia namna kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) inatekeleza Mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

Moja ya wadau hao ni Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dk. Venance Mwasse ambay ametembelea banda la GGML katika maonesho hayo yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Dk. Mwasse alipata maelezo kutoka kwa Ofisa Manunuzi (Mikataba) wa GGML, Silas Shija (wa kwanza kulia) aliyekuwa ameambatana na Scholastica Hoya, Ofisa Rasilimali Watu na Innocent Mushi ambaye ni Ofisa Mwandamizi (Rasilimali Watu).

Walieleza jinsi GGML inavyosaidia miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi katika jamii zinazozunguka migodi yake kama vile elimu, afya, maji, miundombinu na kilimo.

Miradi hiyo inaakisi dhamira ya GGML kwa jamii inayozunguka mgodi kuwa na maendeleo endelevu.Mojawapo ya maadili yake ya msingi, na maono yake ni kutoa mchango chanya.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...