Kampuni ya Sukari Kilombero kupitia bidhaa yake ya Bwana Sukari inatumia fursa ya maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam kuonyesha bidhaa zake na kutoa elimu kwa Watanzania kuhusu fursa zilizopo kutokana na uwekezaji unaofanywa na kampuni katika mradi wake wa Upanuzi.
Kwa mara ya kwanza katika maonesho hayo, wateja wanaweza kujionea sukari zilizo katika paketi ndogo za gramu 50, maarufu kama 'Kitamtam' ambazo zinapatikana kwa bei ya reja reja ya shilingi 200/-.

Baadhi ya wateja waliofika katika banda la Kampuni ya Sukari Kilombero kujionea bidhaa mbalimbali za Bwana Sukari.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Sukari Kilombero, Olympia Fraten (kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Kampuni hiyo, Fimbo Butallah katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...