Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Bunge la Malawi zilizopo Jijini Lilongwe tarehe 6 Julai, 2023. Kulia ni Makamu wa Rais wa Malawi Dkt. Saulos Klaus Chilima akiwa pamoja na Spika wa Bunge hilo Bi. Fiona Kalemba kushoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipanda mti nje ya Ofisi za Bunge la Malawi kama kumbukumbu wakati alipofanya ziara Ofisini hapo Jijini Lilongwe nchini Malawi tarehe 6 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Malawi na Baba wa Taifa hilo Hayati Dkt. Kamuzu Banda lililopo katika Makumbusho ya Kamuzu, Lilongwe nchini Malawi tarehe 6 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mama Cecilia
Kadzamira ambaye alifanya kazi kwa karibu na Rais wa Kwanza wa Malawi na Baba
wa Taifa hilo Hayati Dkt. Kamuzu Banda wakati alipokuwa akitoka kwenye
Makumbusho ya Kamuzu, Lilongwe nchini Malawi tarehe 6 Julai, 2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...