Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, ndugu Sarah Mwaipopo amefungua mafunzo ya kujenga uelewa kwa wajumbe wa Kamati ya Ukaguzi na Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OWMS) kuhusu majukumu ya Kamati ya Ukaguzi

Mwaipopo amefungua mafunzo hayo mkoani Morogoro yanayofanyika kwa siku mbili kwa wajumbe wa Kamati hiyo ili kuhakikisha kuwa Kamati inaifahamu taasisi ili kuweza kumshauri Afisa Masuuli na wajumbe wa Menejimenti ili kuweza kuleta tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ambapo amesema kuwa Kamati hiyo ni jicho la taasisi

‘’Kamati ya Ukaguzi ni jicho la taasisi na chombo muhimu katika uendeshaji wa taasisi ili kuhakikisha kuwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za Serikali na Kamati ifanye kazi kwa uhuru, Menejimenti ya OWMS iiwezeshe Kamati ya Ukaguzi kutekeleza majukumu yake ; kuwa na uelewa wa pamoja ; na kushirikiana,’’ amefafanua Mwaipopo.

Pia, ameongeza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Ukaguzi na wa Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ili kupata uelewa wa majukumu ya Kamati ya Ukaguzi; mahusiano baina majukumu ya Kamati ya Ukaguzi na Menejimenti ; majukumu ya Mkaguzi wa Nje na ya Mkaguzi wa Ndani ; kupata uelewa ili kuweza kusimamia na kudhibiti vihatarishi.

Mwaipopo ameipongeza Kamati ya Ukaguzi kwa kazi nzuri inayofanya ya kuisimamia na kushauri OWMS katika uendeshaji wa taasisi na inaiwezesha OWMS kupata hati safi

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi wa OWMS, Dkt. Omari Fadhil amemshukuru Mwaipopo kwa kuona umuhimu wa kuwezesha mafunzo hayo kufanyika na kwa niaba ya Kamati tutaendelea kukupa ushirikiano ili OWMS iendelee kupata hati safi na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria, taratibu na na kanuni na tutoe ushirikiano kwa Mkaguzi wa Nje, Mkaguzi wa Ndani na Kamati ya Ukaguzi

Mafunzo yanatolewa na Dkt. Mwamba Jingu, Mkufunzi kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha na yanaratibiwa na Joan John, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Ofisi hiyo.


Imetolewa na:

Prisca J. Ulomi,
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali,
08 Julai, 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...