Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Felchesmi Mramba ametembelea banda la Maonesho la Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba Dar es Salaam, na kushuhudia rekodi za kipekee zilizowekwa na kampuni hiyo kutoka mkoani Geita.
Katika maonesho hayo, GGML inajivunia kushiriki kwa mara nyingine tena huku ikiwa imenyakua tuzo ya Kimataifa ya masuala ya Usalama kazini (Global Safety Awards) pamoja na utekelezaji wa miradi kemkem ya inayoinufaisha jamii ya Watanzania.
Maonesho ya Saba Saba ambayo ni fursa kwa Tanzania kushuhudia matunda ya mafanikio yaliyotekelezwa katika nyanja mbalimbali pia yanatajwa kuwa fursa ya kusherehekea maendeleo ya sasa na kuangalia malengo ya taifa ya baadae.

Meneja Usalama kazini kutoka GGML, Isack Senya (wa pili kulia) akimpatia maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba namna Kampuni ya AngloGold Ashanti - Geita Gold Mining Limited ilivyoweka rekodi ya kunyakua tuzo ya kimataifa kwenye masuala ya usalama kazini (Global Safety Awards).


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...