Na Said Mwishehe, , Michuzi TV- Itilima
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana, amesema kazi ya Serikali ni kutengeneza miundombinu na fursa za watu kujiendeleza.
Akizungumza na Waganga wa Tiba Asiili Wilayani Itilima mkoani Simiyu ambapo licha ya kuwapongeza kwa kazi nzuri wanazofanya katika kushiriki kwenye shughuli za maendeleo, ametumia nafasi hiyo kuelezea namna serikali inavyoweza kutengeneza mazingira mazuri ya watu kushughulika na shughuli mbalimbali za kiuchumi.
“Watu wanajiendeleza wenyewe, kazi ya serikali ni kutengeneza mazingira mazuri kwa wananchi kutafuta fursa wajiendeleze kama ni kilimo, kama ni biashara, kama ni ujasiriamali, kama nia ajira, kila mtu kwa nafasi yake anajiendeleza mwenyewe , hakuna mtu anayemuendeleza mwingine,” amesema.
Pia mesema kazi ya serikali kuu, serikali za mitaa ni kutengeneza mazingira mazuri kwa watu kufanya shughuli zao kama ni kilimo waweze kufanya shughuli zao kwa urahisi kwa ufanisi.
“Kama ni biashara ndogondogo waweze kufanya biashara zao bila kero, bila usumbufu , bila kufuatwafuatwa na bila kuwekewa vizingiti katika biashara zao,”amesema.
Ameongeza kama ni biashara kubwa, tengeneza fursa nzuri za kuweza kufanyabiashara zao, ziwe za uhuru zaidi, kila inapotengeneza fursa nzuri, serikali inapotengeneza fursa nzuri watu wanakuwa na uhuru mkubwa wa kutumia akili zao, maarifa yao, na juhudi zao kujiendeleza.
“Jambo hili limekuwepo tangu Awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Julius Nyerere na ndio hivyo hivyo hadi leo chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Ninyi ni mashahidi tangu Rais ameingia madarakani kazi moja kubwa aliyoifanya ni kupanua uhuru.
“Ni uhuru wa watu kufanya shughuli zao , uhuru wa kutoingiliwa , uhuru mkubwa wa kuabudu , uhuru wa kusema , uhuru wa kutoa maoni , uhuru wa kwenye makundi bila kuingilia ilimradi bila kuvunja sheria na Katiba ya Nchi.
“Ninyi ni mashahidi Tanzania ya leo kuna uhuru mkubwa sana, watu wana nafasi kubwa ya kufanya shughuli zao, haki imepanuliwa , haki ya kuishi inaheshimiwa, haki ya kutoa maoni …
“Haki ya kusikilizwa imeheshimiwa ndio maana watanzania leo wana nafasi kubwa zaidi ya kutoa maoni yao kuliko ilivyokuwa siku za nyuma,”alisema Kinana
Amesisitiza maendeleo hayaletwi na mtu kwa mtu mwingine wala Serikali haieleti maendeleo bali inashughulika na maendeleo kwa kujenga miundombinu inayorahisisha mwananchi kufanya shughuli zake kwa urahisi zaidi.
"Serikali kazi yake ni kujenga barabara usafiri inakuwa rahisi, kujenga kituo cha afya ili kuboresha afya ya mwananchi, ikijenga shule wananchi wanasoma na kuwa na elimu nzuri zaidi.
“Wanapata fursa pana zaidi ya kujiendeleza.Kwa hiyo maendeleo yanatokana na wewe mwenyewe, .nataka niipongeze Serikali ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Rais wetu Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupanua fursa, kuwa Serikali inayosikiliza , ili wananchi waweze kujiendeleza,”alisema Kinana.
Kuhusu waganga wa tiba za asili Kinana amewapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa jamii na moja ambalo limemfurahisha ni kwa waganga hao wanakwenda kisasa, wanakwenda na wakati.
“Watoto wenu wanakwenda shule, wamesoma , wanafanya kazi katika Serikali na katika jamii lakini vile vile ninyi wenyewe mnajitoa kuleta maendeleo ya jamii.
“Mnajenga shule, vituo vya afya, kituo cha polisi ndio maana nimesema kuna tofauti kati ya Wachawi na Waganga wa Tiba Asili.Kama mngeitwa Wachawi msingekuwa na haja ya kituo cha polisi kwasababu yale yanayofanywa na Polisi mngemaliza wenyewe.
“Lakini kwasababu ni Waganga wa Tiba Asili yanapofika mambo yanayohusu polisi, amani na utulivu mnaona kuna umuhimu kubwa kujenga kituo cha polisi.Mnashiriki kikamilifu katika shughuli za jamii,”amesema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...