Na Mwandishi Wetu, Babati

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana, amewaomba wana CCM nchi nzima kutambua kuwa kila mema yanayoonekana katika maeneo yao ni maelekezo, maagizo na ahadi zinazotokana na Chama hicho.

Hivyo sifa zote ambazo zinatokana na utekelezaji wa mema hayo lazima zihusishwe na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na Chama Cha Mapinduzi ambacho yeye ndiye Mwenyekiti wake.

Akizungumza leo Julai 24, 2023 wakati wa kikao cha ndani cha Chama Mkoa wa Manyara, Kinana ametumia nafasi hiyo kusisitiza sifa ni lazima ziende kwa CCM  kwa sababu ndio inayokwenda mbele ya wananchi kuomba kura.

“Tukijenga shule inatokana na Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa na sera nzuri pamoja na  ahadi zinazotekelezeka, kwa hiyo mafanikio lazima yahusishwe na Ilani na sera za Chama Cha Mapinduzi.

“Msisahau Chama Cha Mapinduzi kinaongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na serikali inaongozwa na Rais Samia, kwa hiyo ni mafanikio ya Chama chini ya uongozi wa Rais Samia, ni vema katika mafanikio hayo mkamtaja Rais, lakini msisahau kuitaja CCM,” amesema Kinana.

Aidha, amewapongeza wana CCM kwa kukiimarisha Chama huku akikumbusha kila moja kufahamu kuwa Chama kinatokana na wanachama na viongozi wake hawajiteui bali huchachaguliwa na hutokana na wanachama.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...