*Assemahle ampania Twaha Kiduku *

Na.Khadija Seif,Michuziblog

BONDIA wa Ngumi za kulipwa nchini, Karim Mandonga amesema hana hofu na kelele za mpinzani wake, Moses Golala kutoka Uganda kwa sababu amejipanga kumchakaza na kupata ushindi katika pambano la 'Dozi Kubwa'.

Pambano hilo lisilo la Ubingwa la raundi nane litafanyika Jumamosi katika Ukumbi wa Malaika Mkoani Mwanza, huku pambano Kuu (main card) atacheza bondia, Twaha Kassim 'Kiduku' dhidi ya Assemahle wallem kutoka nchini Afrika kusini.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo, Mandonga anasema mpinzani wake amekuwa na maneno mengi tofauti na mabondia aliowahi kucheza nao.

"Golola ndio bondia pekee mwenye kelele nyingi nje ya ulingo, siku ya Jumamosi ndiyo atanifahamu Mandonga ni mtu wa namna gani, "alisema Mandonga.

Upande wa bondia, Golola amekiri kumfahamu mpinzani wake ( Mandonga) kwa ngumi aina ya pelesu na kuhaidi ataonyesha burudani nzuri siku hiyo.

Naye, Twaha Kiduku amesema kuwa amekutana na mabondia wazuri Ila kwake ni bondia wa tofauti, hivyo mpinzani asubilie kichapo kutoka kwake.

Mpinzani wa Twaha Kiduku, Asemahle  amesema amekuja nchini Tanzania kuchukua Mkanda huku akiweka wazi rekodi zake za kutisha na kusema Kiduku ajiandae kukutana na ngumi za Kijana mwenye njaa ya Mafanikio.

 Licha ya Mabondia Twaha Kiduku na Mandonga shuka ulingoni mabondia wengine ni Paul Kamata dhidi ya Juma Misumari kutoka Mji Kasoro bahari.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...