Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mcha Hasan Mcha na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Ushoroba wa Kati (Central Corridor), Wakili flory Okandju walioshika mikasi wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa chumba cha Ufatiliaji wa Magari ya masafa marefu ya kubeba mizigio na bidhaa mbaalimbali. Uzinduzi wa Chumba Hicho umefanyika leo Julai 27, 2023 jijini Dar es Salaam.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania wakishirikiana na Ushoroba wa Kati (Central Corrido), wamezindua Chumba cha Ufatiliaji (Control Room) wa magari ya masafa marefu yanayosafirisha mizingo na bidhaa kutoka katika Bandari ya Dar es Salaam kwenda Nchi jilani.
Mfumo huo utasaidia kufatilia mienendo ya madereva wa magari kutoka bandarini, barabarani, yanapovuka boda hadi yanapofikisha mizigo katika nchi za Rwanda, Burundi, Uganda, Malawi na Congo
Akizungumza leo Julai 27, 2023 wakati wa uzinduzi wa chumba hicho, Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mcha Hasan Mcha amesema kuwa ufunguzi wa Chumba cha Ufuatiliaji ni fursa ya kufanikisha biashara katika usafirishaji mizigo na bidhaa mbalimbali kwa kutumia teknolojia iliyopo.
Amesema ufatiliaji wa magari ya masafa marefu yanayobeba mizigo yatasaidia kuongeza ufanisi wa kazi, kuleta urahisi wa kazi kwa uwazi zaidi ambapo zitaleta ufanikishaji wa kazi za Mamlaka ya Mapato Tanzania.
"Tumeandaa kikosi kazi ambacho kitashirikiana na watu wataokuwa katika Chumba cha Ufatiliaji kwajili ya kufanikisha zoezi la uangalizi wa mizigo ya Masafa marefu." Amesema Mcha Hasan Mcha
Amesema katika kutekeleza hilo pia utaongeza na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji, kuongeza uchumi wa nchi na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja.
Pia amesema kuwa wanampango wa kushirikiana na TANROADS ili waweze kuunganisha mifumo pale inapotokea magari yamepita katika barabara ili kupata taarifa za magari yaliyopita katika vituo vilivyopo.
Pia amewashukuru wafanyakazi TPA, wadau waliosaidia katika kutoa mawazo, maoni ambayo yamefanikisha utengenezaji wa chumba maalumu kwaajili ya kufatilia magari yanayosafirisha mizigo na bidhaa mbalimbali kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi nchi jilani.
Aidha ametoa wito kwa taasisi mbalimbali za serikali kuwa na ushirikiano ili kuweza kuwahudumia wateja ambao wanatumia bandari ya Dar es Salaam na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.
Akizungumzia uzinduzi wa Chumba cha Ufatiliaji, Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Ushoroba wa Kati (Central Corridor), Wakili flory Okandju amesema kuwa kulikuwa na changamoto katika ushafirishaji wa bidhaa na mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda nchi za jilani.
Amesema upotevu wa magari, bidhaa na mizigo mbalimbali njiani au magari kurudi na mizigo nchini, uzinduzi wa chumba hicho ni mwarobainj wa matatizo yote pia kitasaidia kufatilia magari pamoja na dereva ili kufikisha mzigo kwenye nchi iliyotarajiwa na si vinginevyo.
"Sisi Central Corridor tutafatilia mzigo kutoka bandari Dar es Salaam kwenda boda, tutaweza kuona dereva amechukua mzigo gani ndani ya kontena, unaenda wapi, umeondoka Tanzania Saa ngapi, kwanini haujaondoka Tanzania pia kama dereva amesimama anashughuli zake binafsi tutampigia simu ili tufahamu kwanini amesimama." Ameeleza Wakili Okandju
Amesema kuwa wameshatenga fedha kwa mwaka wafedha wa 2023/2024 kwaajili ya kununua Vishkwambi 40 na kuwakabidhi TRA ili ziweze kusaidia utendaji wa kazi.
Amesema kuwa mfumo uliopo katika chumba hicho utaonesha mafanikio na maendeleo makubwa, pia utaboresha biashara katika nchi jilani kupitia teknolojia.
Kwa Upande wa Rais wa Chama cha Wakala wa Forodha (TAFA), Edward Urio amesema Mwanzo kulikuwa na Upotevu wa mzigo njia lawama zilikuwa ni kwa wakala wa Forodha, amesema kwasasa mfumo utasaidia wakala wa forodha, kufuatilia namna unavyokwenda na unasaidia kujitoa katika lawama za upotevu wa mali.
Licha ya hayo amesema kuwa mfumo huo utapunguza upotevu wa mizigo na bidhaa mbalimbali na utaongeza pato la serikali kupitia kodi za forodha.
Kwa Upande wa Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mkurugenzi Mkuu wa Tehama TPA, Abdulatif Minhaji amesema kuwa wapoteyari kwenye kazi yeyote inayohusu masuala ya biashara katika utendaji kazi wa TRA.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mcha Hasan Mcha akizungumza leo jijini Dar es Salaam Julai 27, 2023 kabla ya uzinduzi wa chumba cha Ufatiliaji wa Magari ya masafa marefu ya kubeba mizigio na bidhaa mbaalimbali.
Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Ushoroba wa Kati (Central Corridor), Wakili flory Okandju akizungumza leo jijini Dar es Salaam Julai 27, 2023 kabla ya uzinduzi wa chumba cha Ufatiliaji wa Magari ya masafa marefu ya kubeba mizigio na bidhaa mbaalimbali.
Mkurugenzi Mkuu wa Tehama TPA, Abdulatif Minhaji akizungumza leo jijini Dar es Salaam Julai 27, 2023 kabla ya uzinduzi wa chumba cha Ufatiliaji wa Magari ya masafa marefu ya kubeba mizigio na bidhaa mbaalimbali.
Rais wa Chama cha Wakala wa Forodha (TAFA), Edward Urio akizungumza leo jijini Dar es Salaam Julai 27, 2023 kabla ya uzinduzi wa chumba cha Ufatiliaji wa Magari ya masafa marefu ya kubeba mizigio na bidhaa mbaalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...