NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
MAENDELEO Bank imepata faida ya shilingi milioni 889 kwa kipindi cha Januari mpaka tarehe 30 Juni 2023 ikilinganishwa na shilingi milioni 754 kwa kipindi kama hicho cha mwaka 2022, ikiwa ni ongezeko la asilimia 17.
Mapato ya Uendeshaji wa benki yaliongezeka kwa asilimia 11 hadi shilingi bilioni 1. 20 kutoka shilingi bilioni 1.10 kipindi kama hiki mwaka 2022. Ukuaji huo ulitokana na ongezeko la asilimia 12 ya mapato ya jumla ya riba, na asilimia 27 ya ongezeko la mapato yasiyo ya riba.
Ameyasema hayo leo Julai 30,2023 Mkuu wa Idara ya Biashara- Maendeleo Bank, Bw.Emmanuel Mwaya wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es Salaam.
Bw. Mwaya amesema matokeo hayo yametokana na ukuaji mzuri wa mikopo kwa wateja wadogo na wa kati, pamoja na kupungua kwa mikopo chechefu kutoka asilimia 7 kufikia 4.81 ukilinganisha na kiwango cha udhibiti cha soko ambacho ni asilimia 5.
"Katika kipindi hiki Maendeleo Bank imerekodi ukuaji wa mizania kwa asilimia 4 kutoka shilingi bilioni 101.20 mwezi Juni 2022 hadi shilingi bilioni 114.20. Ukuaji huo ulisababishwa na ukuaji wa asilimia 15 wa amana za wateja hadi shilingi bilioni 81.5 kutoka shilingi bilioni 70.60 zilizoripotiwa mwaka 2022". Amesema Bw. Mwaya.
Aidha amesema kuwa Kutokana na jitihada mbalimbali, Benki iliendelea kukamata masoko kwa bidhaa na huduma bunifu, hivyo kupelekea ukuaji endelevu katika mapato na faida.
"Tuliendelea kufanyia kazi changamoto za wateja ili kuboresha utoaji wetu wa huduma na kuhakikisha tunawapa uzoefu uliobora zaidi pindi watumiapo huduma zetu". Amesema
Pamoja na hayo amesema kuwa Benki inayo matawi 4 na wanategemea kufungua tawi lingine moja eneo la Mbagala na kufanya idadi ya matawi kufika 5 kwa Dar es Salaam, benki ina mawakala zaidi ya 1,400 waliosambaa katika mikoa 11 ya Tanzania. Benki imejiunga na Umoja Switch, hivyo kuiwezesha kutoa huduma za ATM zaidi ya 280 zilizo sehemu mbalimbali za nchi.
Kuhusu mipango ya mbeleni amesema kuwa Benki imepania kuendelea kuimarisha vichocheo vya ukuaji, na kujenga misingi imara ya uendelevu. Mwaka wa fedha wa 2023 ni mwaka wa pili wa mkakati wa muda wa kati wa Benki utakaoishia Mwaka 2026 ambao una jukumu muhimu katika kuimarisha utendaji, na kuipa msingi mzuri benki katika kukabiliana na siku zijazo.
Mkuu wa Idara ya Biashara- Maendeleo Bank, Bw.Emmanuel Mwaya (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Julai 30,2023 katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Idara ya Biashara- Maendeleo Bank, Bw.Emmanuel Mwaya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Julai 30,2023 katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es Salaam
.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...