Na Nasra Ismail ,GEITA
Mkuu wa mkoa wa geita Martin Shigela leo amefungua tawi la bank ya Tanzania Commercial Bank(TCB) Mkoani humo ikiwa ni katika harakati za kupanua wigo wa biashara na kufungua fursa mbalimbali katika mkoa huo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo Shigela alisema kuwa kufunguliwa kwa tawi hilo kumewezesha kupatikana kwa ajira kwani takribani watumishi 800 wameajiriwa katika tawi hilo.
Aidha shigela aliongeza kuwa benki hiyo itawezesha wafanyabiashara wadogowagogo na vikundi vidogovidogo kupata mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha wafanyabiashara hao kuendelea kukuza mitaji yao.
“Sisi wana Geita tutafaidika na mikopo hii, na riba yake ni miongoni mwa riba nzuri kuliko benki zingine, utapewa riba nzuri na muda wa kutosha kuzalisha fedha yako na kuirudisha”Alisema Shigela.
Nae mkurugenzi mtendaji wa TCB Sabasaba Moshingi alisema kuwa kwa kipindi cha miaka 10 bank imeuza mali za bank kutoka bilioni 121 hadi kufikia trillion 1 na bilioni 400 na kuongeza idadi ya matawi kutoka 30 hadi kufikia matawi 80 hivyo kuongeza ajira kutoka wafanyakazi 400 hadi kufikia wafanyakazi 1200.
Kwa upande wake meneja wa TCB Andrew Mzirai alisema kuwa TCB imejipanga kutoa fursa pia kwa wachimbaji wadogowadogo kwa kuwapa mikopo kwa ajili ya vifaa vya kufanyia shughuli za uchimbaiji
Nao wananchi na wadau wa mkoani humo wameishukuru bank hiyo kuanzisha tawi hilo kwani litawasaidia kuwapa huduma kamilifu kwa ghalama nafuu hasa wafanyabiashara na wastaafu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...