Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (wa tatu
kulia) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga ameendelea
kuwafikia Wajasiriamali Mkoani Shinyanga ambapo leo ilikuwa zamu ya Mama
Lishe Manispaa ya Shinyanga kupatiwa msaada wa Majiko ya Gesi 165 yenye
thamani ya Shilingi Milioni 8.2 kwa ajili ya kuwarahisishia kazi katika
shughuli zao na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa utunzaji
mazingira kwa kutumia nishati mbadala.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi majiko 165 yakiwa yamejazwa gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya
Shinyanga leo Ijumaa Julai 7,2023 katika ukumbi wa CCM Wilaya ya
Shinyanga Mjini, Mhe. Mayenga amesema lengo lake ni kuwafikia akina mama
wajasiriamali 800 katika wilaya zote za mkoa wa Shinyanga.
“Tayari
nimetoa majiko 250 kwa Mama Lishe Wilayani Kahama yenye thamani ya
shilingi Milioni 12.5 , na Majiko ya Gesi kwa Mama Lishe 165 Shinyanga
Mjini yenye thamani ya shilingi Milioni 8.25 na nitaendelea kutoa majiko
ya gesi katika wilaya zote za Mkoa wa Shinyanga lengo ni kuwafikia
wanawake 800 kwa kuwapatia majiko ya gesi”,amesema Mhe. Mayenga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akizungumza na Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga
“Wajasiriamali
hawa, mama lishe hawa nimewatafuta kwenye maeneo yao ya kazi bila
kuangalia hawa ni wanachama wa CCM ama la kwani lengo langu ni kuona
wanawake wanapata furaha. Hii ni sehemu ya kuonesha upendo kwa
Wajasiriamali na Mama Lishe pamoja kuunga mkono juhudi zinazofanywa na
wanawake katika shughuli za kiuchumi na utunzaji mazingira kwa kutumia
nishati mbadala sambamba kuwapunguzia gharama za kununua mkaa na nishati
zingine”,ameongeza Mayenga.
“Nitaendelea kutoa majiko ya gesi
800 mkoa mzima. Majiko haya tayari yana gesi, nina dhamira ya kutoa kwa
wananchi kile ninachokipata. Mambo mengine tunafanya kwa sababu ya
utashi wetu binafsi lakini pia mambo anayohamasisha Mhe. Rais Dkt. Samia
viongozi tufanye katika kuwaletea maendeleo wananchi. Mhe. Rais Samia
anataka wabunge tufanye kazi ya kusaidia wananchi”,amesema Mhe. Mayenga
Sehemu
ya majiko ya gesi yaliyotolewa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga
Mhe. Lucy Thomas Mayenga kwa wajasiriamali 'Mama Lishe' Manispaa ya
Shinyanga.
Mbunge huyo ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuwa
wazalendo kwa kuwapenda na kuwasemea mazuri. “Tuwapende viongozi wetu,
tuwataje kwa wema, tuwaseme vizuri”.
Kwa upande wake, Mwenyekiti
wa UWT Mkoa wa Shinyanga, Grace Bizulu amempongeza Mbunge Mhe. Lucy
Mayenga kwa moyo wa upendo na wa pekee katika kusaidia wananchi.
“Mnyonge
mnyongeni lakini haki yake mpatie. Kwa kweli Lucy Mayenga ana moyo wa
pekee, ana moyo wa kutoa. Wabunge wote Shinyanga wangekuwa kama Lucy
Mayenga tungefika mbali”,amesema Bizulu.
Katika hatua nyingine
amewataka akina mama kuacha viburi kwa waume zao na kuhakikisha
wanafuata maadili mema na kutunza familia ili kuepuka mmomonyoko wa
maadili unaochochea vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga, Grace Bizulu.
“Tumepoteza
maadili hatufundishi watoto tuko Busy na majukumu watoto wanaharibika.
Naomba tufanye majukumu ya kutafuta pesa na kutunza familia lakini pia
Wanawake tusiwe na kiburi, lazima tufuate maadili, tuheshimu waume zetu
kisa tuna vipato kuwazidi akina baba. Watoto wetu wanadanga, wamekuwa
mashoga kwa sababu ya kukosa maadili”,amesema Bizulu.
Mwenyekiti
wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini, Rehema Nhamanilo amesema Mbunge Lucy
Mayenga anapaswa kupongezwa kutokana na mambo makubwa ambayo amekuwa
akiyafanya kuwasaidia wananchi.
“Mhe. Lucy Mayenga amekuwa akifanya mambo makubwa, anafanya vitu vya ajabu ambavyo hatujavizoea kuviona”,amesema Nhamanilo.
Katibu
wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ally Majeshi amesema kitendo
alichofanya Mbunge huyo kuwakumbuka mama lishe kinapaswa kuigwa kwani
kimewapa raha akina mama.
“Haya ndiyo mambo ya wabunge wa CCM
kuwapa raha watu waliowachagua badala ya kuwapa mawazo au manung’uniko.
Mhe. Lucy Mayenga umefanya jambo zuri, huu ndiyo uimara na umahiri
ulionao ndani ya CCM. Mambo mazuri unayofanya yanawafanya wananchi
wakipende Chama Cha Mapinduzi. Tunataka CCM ilelewe na wenye kujituma na
kujitoa”,amesema Majeshi.
Nao Mama Lishe hao waliopata majiko ya
gesi wamemshukuru Mbunge huyo kwa kuwapatia majiko hayo ya gesi ambayo
yatasaidia katika kazi zao lakini pia kutunza mazingira huku pia
wakimshukuru kwa kuleta Madaktari Bingwa wa Macho ambapo wananchi wa
Mkoa wa Shinyanga walipata huduma bure.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akipokelewa
kwa shangwe na akina mama wajasiriamali 'Mama Lishe' Manispaa ya
Shinyanga alipowasili katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini kwa
ajili ya kutoa msaada majiko ya gesi 165 kwa Mama Lishe hao. Picha na
Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akipokelewa
kwa shangwe kwa kubebwa na akina mama wajasiriamali 'Mama Lishe'
Manispaa ya Shinyanga alipowasili katika ukumbi wa CCM Wilaya ya
Shinyanga Mjini kwa ajili ya kutoa msaada majiko ya gesi 165 kwa Mama
Lishe hao.
Mama Lishe wakipiga picha (Selfie) na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akizungumza
na wajasiriamali 'Mama Lishe' Manispaa ya Shinyanga ambapo amewapatia
majiko ya gesi 165
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akizungumza
na wajasiriamali 'Mama Lishe' Manispaa ya Shinyanga ambapo amewapatia
majiko ya gesi 165
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akizungumza
na wajasiriamali 'Mama Lishe' Manispaa ya Shinyanga ambapo amewapatia
majiko ya gesi 165
Sehemu
ya majiko ya gesi yaliyotolewa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga
Mhe. Lucy Thomas Mayenga kwa wajasiriamali 'Mama Lishe' Manispaa ya
Shinyanga
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (wa nne
kulia) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (wa pili

wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kushoto)
akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Mmoja
wa Mama Lishe akitoa neno la shukrani baada ya Mbunge wa Viti Maalumu
Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga kukabidhi majiko ya gesi kwa
Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Mmoja
wa Mama Lishe akitoa neno la shukrani baada ya Mbunge wa Viti Maalumu
Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga kukabidhi majiko ya gesi kwa
Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga, Grace Bizulu akizungumza wakati
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga
akigawa majiko ya gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Katibu
wa UWT Mkoa wa Shinyanga, Asha Juma Kitandala akizungumza wakati Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akigawa
majiko ya gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Katibu
wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini, Sharifa Hassan Mdee akizungumza
wakati Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga
akigawa majiko ya gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti
wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini, Rehema Nhamanilo akizungumza wakati
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga
akigawa majiko ya gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Katibu
wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ally Majeshi akizungumza wakati
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga
akigawa majiko ya gesi kwa Mama Lishe Manispaa ya Shinyanga.
Sehemu ya Mama Lishe/Wajasiriamali wakiwa kwenye mkutano na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga

Sehemu ya viongozi wa UWT wakiwa kwenye mkutano na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga
Sehemu ya viongozi wa UWT wakiwa kwenye mkutano na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga
Picha ya kumbukumbu Wajasiriamali na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga

Picha za kumbukumbu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...