Na Mwandishi Wetu, Mwanga,
MBUBGE wa Jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro Joseph Tadayo ameshiriki tamasha la kuchangia vyombo vya muziki katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kirya lililopo Kata Kirya wilayani humo.
Akizungunza wakati wa tamasha hilo Mbunge Tadayo pia ametumia nafasi hiyo kutoa taarifa fupi ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika Kata Kirya ikiwemo mradi mkubwa wa kilimo cha mwangiliaji Kambi ya Swala,mradi kituo cha afya cha kisasa, Ofisi ya Masijala ya ardhi ,mradi mkubwa wa maji ,barabara pamoja na miradi ya Elimu.
Pia ametembelea na kukagua ujenzi wa msikiti wa Mangulay ambapo kipindi kilichopita alichangia na baadae akachangia tena na akiwa kwenye ujenzi huo wa msikiti ameahidi kuendelea kuchangia mpaka pale utakapo kamilika.
Ujenzi wa msikiti huo ambao ulidumu kwa zaidi ya miaka tisa kwasasa umefikia hatua za kukamilika baada mbunge huyo kuendelea kufuatilia na kuahidi kuendelea kuchangia kila hatua wananchi wafanye ibada sehemu nzuri.
"Ibada sehemu muhimu katika maisha mwanadamu kuwa hofu ya Mungu na kuzalisha Taifa yenye maadili bora na ili Taifa lipige hatua kimaendeleo inahitaji jamii yenye uadilifu na uaminifu.
"Tunawashukuru sana viongozi wa dini kwa kuendelea kulibeba Taifa na viongozi kwa ujumla katika maombi, hivyo sisi tunaahidi kuendelea kuimarisha ushirikinao ili tujenge taifa letu kwa pamoja,"amesema Tadayo.
Awali akiongoza ibada Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mwanga Chediel Sendoro ameiasa jamii kupendana na kuacha kuwaonea wanyonge." Kama amri ya Mungu inavyoelekeza mnapaswa kupendana na kutowaonea wengine na kutenda haki."
Kwa upande wake Shekhe wa Msikiti wa Mangulay Amri Shabani Kabavako amemshukuru Mbunge kwa kuona umuhimu wa kuchangia ujenzi wa msikiti huo ambao ujenzi wake ulisimama kwa muda mrefu kwa kushindwa kuundeleza kutokana na uhaba wa fedha.
"Msikiti huo ni wa muda mrefu sana ni zaidi ya miaka tisa tulishindwa kuendelea mvua zikinyesha hatuwezi kufanya ibada na jua pia likiwaka tunashindwa kufanya ibada.Tunamshukuru Mbunge wetu alikuja mara ya kwanza akachangia laki tano na leo tena kachangia laki tatu, hatuna budi kumshukuru,"amesema.
Home
JAMII
MBUNGE MWANGA ASHIRIKI TAMASHA KUCHANGIA VIFAA VYA MUZIKI KKKT KIRYA, KUCHANGIA UJENZI MSIKITI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...