Na WILLIUM PAUL, MOSHI.
KATIKA kuhakikisha wakulima wa zao la ndizi katika Jimbo la Moshi vijijini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wananufaika na Kilimo hicho Mbunge wa Jimbo hilo Prof. Patrick Ndakidemi ameamua kugawa miche ya kisasa ya migomba.
Miche hiyo aina ya Kimalindi ni ya kisasa na kuwa imekuwa ikizaa na kutoa mazao yenye tija ikilinganishwa na aina ya migomba kama hiyo iliyopo hivi sasa ambayo imeonekana kutokufanya vyema kwa wakulima.
Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi amesema kuwa miche hiyo tayari ameigawa kwa wakulima katika maeneo mbalimbali na kuwa imekuwa na uwezo wa kuvumilia magonjwa mbalimbali ya migomba tofauti na iliyopo hivi sasa.
'Leo naenda kukutana na madiwani wangu zaidi ya 20 na ninaenda kugawa aina hii mpya ya miche zaidi ya 100 ambayo wataenda kuiotesha katika maeneo yao na zoezi hili ni endelevu'amesema Prof Ndakidemi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...