Na Albano Midelo,Songea
SERIKALI inatarajia kuanza kujenga barabara ya mchepuko kilometa 16
katika mji wa Songea ili kukabiliana na kero ya malori 1000 ya makaa ya
mawe yanayopita mjini Songea kwa siku.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi
Godfrey Kasekenya wakati anajibu ombi la wananchi wa Kata ya Lilambo
Manispaa ya Songea la kuomba kujengewa barabara itakayopita nje ya mji
ili kuepuka kero ya malori ya makaa ya mawe.
Naibu Waziri huyo amekiri kuwa barabara ya Songea hadi Makambako hivi
sasa inabeba mizigo mingi na mizito hivyo serikali mwaka huu imeamua
kuifanyia matengenezo makubwa kwa kuijenga upya ili iwe barabara ya
kisasa.
“Mwaka huu tutaanza kujenga barabara ya lami kuanzia Lutukira sehemu
ambayo imechoka sana hadi Songea mjini,ikiwa ni Pamoja na kujenga
barabara ya mchapuko Songea mjini yenye urefu wa kilometa 16’’,alisema
Naibu Waziri.
Amesema barabara hiyo ya mchepuko itasaidia magari makubwa kupita
nje ya nchi badala ya kupita katikati ya mji na kwamba barabara za
mchepuko zitapita sehemu tatu ambazo amezitaja kuwa ni eneo la
Namanditi,Msamala na Sogea .
Amesema serikali imefanya tathmini ya fidia kwa wananchi wote
waliopitiwa na barabara ya mchepuko ambapo tayari serikali imeandaa
fedha za kuwalipa fidia zaidi ya shilingi bilioni nne ambazo zipo tayari
hazina.
Hata hivyo amesema wakati ujenzi wa kipande hicho unaendelea serikali
itaendelea kutafuta fedha za ujenzi wa kipande cha barabara ya kutoka
Lutukira hadi Makambako.
Amesema licha ya serikali kutoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 37 za
upanuzi na ukarabati wa uwanja wa ndege wa Songea,mwezi Septemba
mwaka huu serikali italeta gari la kisasa za Zimamoto kwa ajili ya uwanja
wa ndege wa Songea.
Mbunge wa Songea mjini na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt.Damas
Ndumbaro kwa niaba ya wananchi wa Songea ameishukuru serikali kwa
kutenga bajeti katika mwaka huu wa fedha kujenga barabara ya mchepuko
inayokwenda sanjari na ujenzi wa barabara mpya ya lami kutoka Songea
hadi Lutukira kilometa 100.
“Kwa siku moja katika mji wa Songea malori 1000 yenye makaa ya mawe
yanapita mjini Songea,barabara hii katikati ya mji wa Songea imekuwa kero
na haiwezekani tena,tunaishukuru serikali kwa kutenga fedha mwaka huu
ili kuanza ujenzi’’,alisema.
Naye Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
akizungumza na wananchi wa Songea alipofanya ziara ya kikazi mkoani
Ruvuma alisema amesafiri kwa njia ya barabara toka Dodoma hadi Songea
na ameiona hiyo barabara ilivyochoka na kuchakaa hivyo serikali mwaka
Miongoni mwa malori ya makaa ya mawe yakiwa katikati ya mji wa Songea,serikali inajenga barabara ya mchepu ili malori yote yasiingie katikati ya mji na kusababisha foleni kubwa ya magari katikati ya mji wa Songea.
Katikati mwenye kipaza sauti ni Mbunge wa Songea mjini ambaye pia ni Waziri wa Sheria na Katiba Dkt.Damas Ndumbaro.Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya akizungumza na wananchi wa mji wa Songea kuhusu mpango wa serikali mwaka huu kuanza kujenga barabara ya mchepuko yenye urefu wa kilometa 16 mjini Songea ili kuyawezesha magari makubwa kutoingia katikati ya mji ambapo amesema ujenzi wa barabara hiyo ya mchepuko unakwenda sanjari na kuanza ujenzi wa barabara ya Songea -Makambako kipande cha Songea-Lutukira chenye urefu wa KM 100.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...