Na Mwandishi Wetu, Tanga

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Husna Sekiboko amesema katika kipindi kilochobaki kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 wataendelea kuboresha na kutatua changamoto zilizopo katika maeneo yote ya mjini na vijijini.

Ametoa ahadi hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni za kumnadi mgombea udiwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) zilizofanyika Kata ya Potwe wilayani Muheza.

Amesema kuwa licha ya kutekeleza baadhi ya miradi katika kata hiyo lakini amekiri kuwepo na changamoto ambazo zinahitaji utatuzi na kwamba ni CCM pekee ndiyo yenye kuweza kumaliza changamoto hizo.

Kata hiyo inafanya uchaguuzi kutokana na Diwani aliyekuwepo Athuman Bahari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema )kuondoka kwenye chama hicho na kujiunga na CCM .

Hata hivyo bahari ndiye Mgombea wa kiti cha udiwani katika Kata hiyo kwa tiketi ya CCM.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...