MAREHEMU FRANCIS LEONARD MTEGA
(01-06-1959 – 01-07-2023)
___________________
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mhe. Francis
Leonard Mtega, Mbunge wa Jimbo la Mbarali (CCM) kilichotokea leo tarehe 01
Julai, 2023 kwa ajali ya kugongwa na Trekta (Power Tiller) shambani kwake
Mbarali, Mkoani Mbeya.
“Nimepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Francis Leonard Mtega. Natoa
pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa, Waheshimiwa Wabunge na Wananchi wa
Jimbo la Mbarali. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika
kipindi hiki kigumu,” amesema Mheshimiwa Spika.
Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya
Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea
kutolewa.
Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali
Pema Peponi, Amina.
Imetolewa na : Kitengo cha Mawasiliano
na Uhusianmo wa Kimataifa
Ofisi
ya Bunge
Dodoma
01 Julai 2023
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...