Na Albano Midelo,Songea

MKOA wa Ruvuma unatarajia kuzindua wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama Duniani,Agosti Mosi,2023 katika Kituo cha Afya kata ya Ruvuma kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen ndaki amesema Tanzania inaungana na nchi nyingine Duniani kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama ambayo itaanza Agosti Mosi hadi 7 mwaka huu.

“Lengo la kuhamasisha unyonyeshaji maziwa ya mama ni kulinda na kuendeleza afua ya unyonyeshaji kama njia mojawapo ya kuboresha hali ya lishe kwa watoto’’,alisisitiza Ndaki.

Hata hivyo amesema kwa mwaka huu wiki ya unyonyeshaji maziwa katika Mkoa wa Ruvuma,itafanyika katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma ambapo ametoa rai kwa viongozi,watendaji na wananchi kushiriki kikamilifu kwenye maadhimisho hayo .

Kaulimbiu ya mwaka huu ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama inasema “Saidia unyonyeshaji,wezesha wazazi kulea Watoto na kufanya kazi zao kila siku’’.

Mpango Jumuishi wa Taifa wa Lishe unalenga kuweka mazingira rafiki yanayomwezesha mwanamke kunyonyesha ili kulinda na kuendeleza unyonyeshaji wa maziwa ya mama.

Kupitia mpango huo serikali na wadau wengine hufanya kazi pamoja kuendeleza, kuhamasisha na kulinda unyonyeshaji watoto maziwa ya mama ili kuimarisha afya ya jamii.

Mpango Jumuishi wa taifa wa Lishe unatambua kuwa unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni jukumu la pamoja linaloenda sanjari na utekelezaji wa sera mbalimbali za nchi zinazosaidia kuboresha afya ya mtoto na jamii kwa ujumla.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki  akizungumzia maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama mkoani Ruvuma ambayo inaanza Agosti Mosi mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...