Na. Damiani Kunambi, Njombe.
Benki ya CRDB imekabidhi vifaa mbalimbali kwaajili ya Zahanati ya Kilondo na shule ya msingi Kilondo vyenye jumla ya thamani ya sh. Mil. 10 na kupokelewa na Mkuu wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Sunday Deogratius.
Akipokea vifaa hivyo ambavyo ni bati 152 kwaajili ya shule ya msingi shikizi Kilondo pamoja na darubini, kitanda cha kujifungulia akina mama wajawazito pamoja na vifaa tiba vinginevyo kwaajili ya Zahanati ya Kilondo mkuu huyo wa wilaya ameishukuru benki hiyo kwa mchango wao huo kwani unaipa nguvu serikali nwenye thamani na wenye kuipa nguvu Serikali katika upande wa huduma za afya na kuboresha miundombinu ya Elimu.
" Napenda nichukue fursa hii kuipongeza benki ya CRDB kwa mchango wao huu katika huduma za maendeleo kwa jamii, ombi langu kwenu na taasisi nyinginezo ni kushirikiana kwa pamoja katika kuleta maendeleo wilayani hapa na hasa katika sekta ya afya na elimu". Amesema Mwnziva.
Imani Mwaisango ni meneja wa benki hiyo tawi la Ludewa ambaye ndiye aliyekabidhi vifaa hivyo amesema wametoa msaada huo ikiwa ni ishara ya ushirikiano mwema baina ya Benki hiyo, Serikali pamoja na Jamii kwa ujumla kwakuwa ni sehemu yao ya kugusa jamii na kuleta chachu ya maendeleo katika kazi zao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...