Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI wa Msama Promotion Alex Msama amewashauri viongozi wa ngazi mbalimbali nchini wakiwemo wabunge wanamuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake anazofanya katika kuhakikisha uchumi wa unakuwa.
Msama ameyasema hayo leo Julai 6, 2023, jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza umuhimu wa viongozi kumuunga mkono Rais Samia ili kuhakikisha jitihada zake za kuleta maendeleo zinafanikiwa.
Amesisitiza kuwa wabunge pamoja na viongozi wengine wanapaswa kuwa imara katika kupeperusha sera nzuri za Tanzania, na hawapaswi kubaki nyuma katika kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia.
“Watu wote wenye nia mbaya na nchi yetu, lazima tupambane nao bila kuwaogopa wala kuwaonea haya. Nchi yetu ni ya kila mtamzania, na ana haki ya kupambana kuhakikisha amani, utulivu na mshikamano tulionao unaendelea kuwepo,"amesema.
Msama amesema Rais anafanya kazi kubwa na mambo mengi yalikuwa hayaendi, lakini sasa mambo yanaenda vizuri sana, wawekezaji wakubwa, wadogo na wa kati wanakuja kuwekeza nchini kwetu.
Amesisitiza hayo yote ni matunda yatokanayo na yeye kutembelea kwenye nchi mbalimbali za kigeni kuunganisha biashara ili kukuza uchumi wa nchi lakini kubwa zaidi ameendelea kuweka utulivu katika sekta mbalimbali na matokeo chanya yanaonekana.
Ametumia nafasi hiyo kueleza katika nchi yetu kila mmoja wetu analo jukumu la kuhakikisha nchi inaendelea kuwa yenye amani, umoja na utulivu huku akisisitiza ni wakati wa kujenga uchimi na kazi hiyo inapaswa kufanya na watu wote chini ya uongozi mahiri wa Rais Samia.
MKURUGENZI wa Msama Promotion Alex Msama akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaama leo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...