KAMPUNI ya Alaf Tanzania imezindua msimu wa tano wa shindano la kupiga picha lijulikanalo kama 'Safal Eye in the wild Photography ' kwa mwaka 2023 kuanzia leo Julai 28 na kumalizika Septemba 15, 2023.

Lengo kubwa la shindano hilo ni kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu uhifadhi wa mazingira kupitia uwezo wa upigaji picha.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam mara baada ya uzinduzi huo uliofanyika jijini Nairobi leo Julia 28, 2023 Mkurugenzi Mtendaji wa Safal Group, Anders Lindgren amesema, kwa kutumia nguvu ya sanaa na ubunifu anaamini Kwa kupita shindano hilo wanaweza kufua mioyo na akili kwa kuhimiza suluhisho la kibunifu na mbinu endelevu za kukabiliana na athari za ukame.

"Majaji wetu watatathmini picha zinazoonyesha athari za ukame, watakuwa wakitafuta picha zinazoibua hisia, kusimulia hadithi za kuvutia na kuwasilisha hitaji la dharura la uhifadhi wa mazingira na suluhisho endelevu ili kupunguza athari mbaya za ukame" amesema Lindgren.

Naye, Meneja Uhusiano wa Alaf Tanzania, Hawa Bayumi amesema, kupitia shindano hilo kutawawezesha na kuhamasisha jamii na wapiga picha kuweza kupiga picha ili kuweka jicho na mtazamo zaidi kwenye mazingira na athari ambayo mazingira yetu imepata kutokana na uharibifu.

Amesema, pia shindano hilo linalenga kukuza ushirikiano wa maana na endelevu na wadau pamoja na jamii katika masoko ya mazingira yaliyojengwa huku pia wakilenga kuanzisha uhusiano wa kina zaidi na Jumuiya za ndani na nje za kampuni.

"Kila mwaka shindano hili huzingatia kipengele cha mfumo ikolojia ili kukuza mjadala na kuonyesha umuhimu wa uhifadhi wa mazingira, kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Ukame'. Ukame unaendelea kuwa na matukio mabaya na makubwa hasa kwa Jumuiya zinazotegemea kilimo katika Kanda. Amesema Bayumi

Ameongeza kuwa, ukosefu wa mvua za kutosha na vipindi vya kiangazi vya muda mrefu vimepunguza mavuno ya mazao, kuongezeka kwa hasara ya mifugo na hivyo kusababisha athari mbaya inayochangia kwa kiasi kikubwa uhaba wa chakula katika jamii.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Safal Group, Sarit Shah ameitaka jamii kujumuika kwa pamoja wakiwa na dhamira moja ya kuongeza uelewa juu ya athari za ukame na kuleta mabadiriko chanya kwa manufaa ya jamii zetu na vizazi vijavyo.

"Katika shindano hili wapiga picha watapata fursa ya kuwa sehemu ya miradi mbalimbali inayolenga kukabiliana na ukame ndani ya jamii ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na tuzo ya dhahabu ya USD 5000, mshidi wa tuzo ya fedha atapata USD 3000 na tuzo ya shamba atapata USD 2000.

Washiriki wote wanaalikwa kuwasilisha picha zao kupitia tovuti maalamu ya shindano hilo kwenye https://safeleyeinthewild.safaelgroup.com/ ifikapo Septemba 15, 2023

Kwa upande wake mmoja wa majaji ambaye aliwahi kuwa mshindi shindano hilo, Daniel Msirikale ameomba wanawake wengi kujitokeza na kushiriki kwa kupeleka picha zao kwani mara nyingi washirika wamekuwa wanaume kuliko wanawake

" Nawahamasisha Wanawake ambao wanapenda kupiga picha wajitokeze na kushiriki shindano hili , kila mtu ajitahidi kupiga picha, kama una simu ama camera we tumia chochote ulichonacho, cha msingi ni kuja na picha yenye ubunifu au utofauti.

. Nawashauri washiriki wa mwaka huu kufuata vigezo na masharti, kama hujaweza kufuata vigezo na masharti baso picha yako itakuwa imetoka mashindanoni, pia jaribu kuleta picha yenye utofauti, picha itakayoshinda ni ile yenye itakayoweza kusisimua watu na kutushtua sisi majaji.

Ameongeza kuwa hakutakuwa na na udanganyifu wowote na wale wapiga picha ambao wataleta picha ambazo sio zao. Amesema ili kuhakikisha picha inayotumwa imepigwa na muhusika basi ni lazima utoe picha halisi uliyopiga kabla haujaedit, tutakuwa na maswali kadhaa ya kuhakikisha kuwa picha ile ni yako.

Baadhi ya wafanyakazi wa wakifatilia Uzinduzi wa msimu wa tano wa shindano la kupiga picha lijulikanalo kama 'Safal Eye in the wild Photography ' kwa mwaka 2023, uzinduzi huo umefanyika Nairobi Nchini Kenya Julai 28, 2023.
Meneja Uhusiano wa Alaf Tanzania, Hawa Bayumi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya Kampuni ya Alaf Tanzania kuzindua msimu wa tano wa shindano la kupiga picha lijulikanalo kama 'Safal Eye in the wild Photography ' kwa mwaka 2023.

Picha ya pamoja ya baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Alaf Tanzania na Mmoja ya majaji wa msimu wa tano wa shindano la kupiga picha lijulikanalo kama 'Safal Eye in the wild Photography ' kwa mwaka 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...