Kupitia Tuzo za umahiri katika Uandishi wa Habari (EJAT) zilizotolewa katika Ukumbi wa Milimani City, Jumamosi ya Julai 22, 2023 ambapo Waandishi wa Habari waliweza kushindana kwenye vipengele mbalimbali, imeelezwa kuwa kuingia kwa Marie Stopes Tanzania kutaongeza Elimu ya masuala ya uzazi kupitia kazi mbalimbali zawashiriki.
Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kushirikiana na Marie Stopes Tanzania (MST) wameingia makubaliano ya miaka miwili wenye lengo la kukuza uandishi wa habari kuhusu afya ya uzazi.
Mkurugenzi Mwandamizi wa Marie Stopes, Dkt. Geofrey Sigalla amesema MST inashirikiana na MCT ili kuendelea kuweka msisitizo na kuchagiza msukumo wa utoaji wa habari zinazohusu afya ya uzazi.
Amesema msukumo uliochangia Marie Stopes kushiriki katika kutambua umuhimu wa Waandishi wa Habari ni kutambua umuhimu wa habari za afya ya uzazi kama sehemu ya haki muhimu zenye mchango kwa jamii.
“Hii ni pamoja na umuhimu uliopo katika masuala haya ni katika kuhakikisha tunakuwa vizazi vyenye afya hivyo Taifa lenye ustawi na linanufaika na idadi ya watu wake na vile vile kuepusha vifo vya akina mama vinavyotokanana uzazi,” amesema Dkt. Sigalla.
Dkt. Sigalla amesema Waandishi wa Habari wanamchango mkubwa katika kuchangia mabadiliko ya kisera, kisheria yenye leongo la kuweka mazingira mazuri ya kisera katika kuhakikisha utapikanaji wa huduma ya afya ya uzazi unakuwa na manufaa kwa wote.
Pia amesema ushirikiano wao na Baraza la Habari Tanzania ni imani yake kuwa mwakani waandishi wengi watashiriki katika kuwasilisha kazi zetu katika kipengele hiki cha afya ya uzazi na hivyo kuongeza ushindani katika habari hizo huku akiwataka waandishi wa habari kuendela kutoa kipaumbele katika kipengele hicho cha afya ya uzazi nchini.
Kwa Upande wake Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga amesema wameingia ushirikiano wa kukuza uandishi wa Habari za Afya ya Uzazi nchini.
“Makubaliano yetu ni ya miaka miwili ambapo kwa pamoja tutakitangaza kipengele cha Afya ya Uzazi ili kuwashawishi kuandika na kuandika kwa umahiri masuala hayo ambayo ni nyeti, hilo ni jambo muhimu kwa kuwa linahusiana na maisha moja kwa moja.
“Unapozungumzia Afya ya Uzazi unazunguzia maisha tangu mtu anapozaliwa, hivyo kwetu ni jambo muhimu sana, tumeshukuru sana kupata sapoti hii ya MCT katika EJAT.
“MST wanasapoti kipengele hicho kwa maana ya kutoa uwezeshaji wa kulipa washindi na mambo mengine yote yanayohusiana na suala hilo, pia tutashirikiana kutoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari ili kuwajengea uwezo wa kuandika kwa umahiri kuhusu suala la Afya ya Uzazi
Katika Tuzo hizo waandishi wa habari walioshinda kwa kuandika taarifa za masuala ya Afya ya Uzazi katika kipengele hicho ni pamoja na:
1. Tuzo ya Habari za Afya ya Uzazi (Magazeti) - Zuhura Said (Zanzibar Leo)
2. Tuzo ya Habari za Afya ya Uzazi (Radio) - Peter Lugendo John (TBC Taifa)
3. Tuzo ya Habari za Afya ya Uzazi (TV) - Dafrosa Ngailo (Azam TV
4.Tuzo ya Habari za Afya ya Uzazi (Mtandaoni) - Festo Charles Lumwe (Dar 24).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...