Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda akikabidhi  Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia)

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenge wa Uhuru umewasili Mkoani Shinyanga ukitokea mkoani Simiyu leo Alhamisi Julai 27,2023 katika shule ya msingi Buganika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambapo utaweka Mawe ya Msingi, kufungua na kuona jumla ya Miradi 41 yenye thamani ya Shilingi 14,027,687,009.20.


Akizungumza wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru leo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema Mwenge wa Uhuru utaweka Mawe ya Msingi, kufungua na kuona jumla ya Miradi 41 yenye thamani ya Shilingi 14,027,687,009.20 mkoani Shinyanga.


Amesema katika Mkoa wa Shinyanga Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa kilomita 571.5 katika halmashauri sita za wilaya ambazo ni Kishapu, Manispaa ya Shinyanga, Halmashauri ya Shinyanga, Manispaa ya Kahama, Msalala na Ushetu.

Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru mkoani Shinyanga zinaanza kukimbizwa katika wilaya ya Kishapu kwa kuzindua,kuweka mawe ya msingi na kuona jumla ya miradi 6 yenye thamani ya Sh.bilioni 1.3.

Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 ni Tunza Mazingira okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa jamii na uchumi wa taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda akikabidhi  Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) . Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda akikabidhi  Hati ya Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia)
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda  Mwenge wa Uhuru.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru
Viongozi mbalimbali Mkoa wa Shinyanga wakifurahia jambo wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika shule ya msingi Buganika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude
 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akipokea Mwenge wa Uhuru
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akipokea Mwenge wa Uhuru

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...