Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
WAZIRI MKUU Mstaafu Mizengo Pinda ameawataka Wakurugenzi, Watendaji na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali nchini kuitumia Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kwamfipa Wilayani Mkoa wa Pwani, kuendelea kujielimisha ili kumpunguzia kazi Mkaguzi na Mdhibiti wa fedha za serikali CAG.
Pinda amesema hayi kwenye ufunguzi wa mafunzo ya 19 ya siku sita kwa Viongozi wa Taasisi na Mashirika ya Umma nchini, katika Shule ya Uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha ambapo amesema kuwa Shule hiyo itumike vizuri kuwajengea uwezo viongozi mbalimbali wa Chama na serikali.
Amesema kuwa viongozi hao waende kusoma katika Shule hiyo ili wajengwe kwa kupigwa msasa wa mara kwa mara ili kumpunguzia CAG kazi kwa viongozi wote kufanya kazi katika malengo ya aina moja.
"Kunatakiwa kuwe na kozi fupi fupi kwa sisi tulio huku serikalini kwani Kuna ubaya gani maDC wote tukutane hapa na viongozi wote wataasisi zinazohusu uendeshaji wa nchi kwa ujumla na mambo yote yanayohusu makatazo kwa kiongozi"
"Wakurugenzi njooni hapa tena wote mmetokana na Chama kinachoongoza piga msasa hawa watu ndipo hautasikia CAG akipiga kelele tena" amesema Mheshimiwa Pinda.
"Nasisitiza uadilifu na kuacha maovu ambayo yanaathiri jamii kwa ujumla ndiyo maana CAG akitoa ripoti yake inakua imejaa madudu mengi yote haya yanatokana na upungufu wa maadili kwa baadhi ya viongozi " amesema Pinda.
"Viongozi wangu katika serikali naomba tuwajibike kikamilifu, kwanza wajibika halafu dai haki yako kila Kiongozi anapaswa kuwa mbunifu katika Taasisi yake na kuwajibika.
"Mashirika makubwa na Taasisi nyingi za serikali nyingi zinayumba sababau Viongozi wengi siyo waadilifu,kitu kinachoitwa uadilifu ni kigumu lakini endapo utakaa na kina baba kama kina mzee Butiku kuna mambo mazuri unaweza kuyapata binafsi naweza sema nimepata bahati ya kuwa na viongozi hawa wakongwe ambao ndiyo walionijenga natumia mfano huu ikiwa ni lengo la kutaka kuwakumbusha umuhimu wa kuthamini wazee katika utendaji wetu" amesema Pinda.
Amesema kuwa wakati umefika sasa kuwajengea uzalendo wananchi huku akitolea mfano wa nchi ya Israel namna ambavyo wamewajengea wananchi wao uipenda na kuithamini nchi yao huku akisema kuwa kila mtanzania anapaswa kuwa mzalendo licha ya kuwa na itikadi tofauti za kidini, kabila na rangi lakini wote wawe kitu kimoja.
Ametoa sifa kwa uongozi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere kuwa licha ya kuwa hakina muda mrefu lakini matunda yake yameanza kuonekana na maua yake yamechanua kutokana na mafunzo waliyopatiwa watu wa kama mbalimbali, viongozi wa ndani na nje ya nchi.
Aidha amriidhishwa na idadi kubwa ya wanawake wanaoshiriki mafunzo hayo "Nimefurahishwa kuona uwiano wa washiriki katika mafunzo haya, idadi iliyopo ya wanaume 27 na wanawake 25 ni idadi nzuri niwapongeze washiriki wote," amesema Pinda.
"Niwaombe viongozi ngazi za serikali tuwe wawajibikaji katika nafasi, sanjari na ubunifu utaowezesha Taasisi zetu kuongeza mapato, hapo hata ukidai nyongeza ya maslahi zaidi tutakuwa na kila sababu ya madai hayo," amesema Pinda.
Aidha Mheshimiwa Pinda ametaka mafunzo hayo yawe endelevu kwa kuanzia vijana mashuleni huku akiwasisitiza Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuwapeleka viongozi wake kuoata elimu ya uongozi katika Shule ya Mwalimu Nyerere ili waweze kujengeka katika misingi bora ya uongozi.
Mstaafu Paul Kimiti amewahimiza viongozi hao kuwa wana haki ya kuwa wazalendo,kutetea haki kutubu yao makosa mbalimbali.
Amesema kuwa hakuna aliyeko juu zaidi ya mwingine hivyo amesisitiza kuwa kuwa kila mmoja anamtegemea mwenzake na kusema kuwa usifanye maaamuzi yoyote bila kushirikisha wenzako wengine hii ndiyo sifa ya Kiongozi bora.
"Kiongozi bora huheshimu anaowaongoza na kuwashirikisha kama ya watu wote anaowaongoza bila ya kujali umri ,itikadi za dini na mambo mengineyo yanayowatofautisha.
Mkuu wa chuo Profesa Marcellina Chijoliga alisema kuwa tangu chuo kianze kimeshapokea washiriki wa kozi 18 na iliyoanza Julai 31 ya 19 zikiwa na washiriki 2019 na kwamba taasisi 40 zimekitumia chuo hicho.
"Kozi iliyopita ilihudhuriwa na washiriki wanawake tu wapatao 71, hii inaonesha ni namna gani wanavyozidi kujiendeleza kielimu kupitia maeneo yao wanayofanyiakazi," alisema Chijoliga.
Katibu Mwenezi wa Siasa mkoani Pwani David Mramba akizungumza kabla ya kumkaribisha Pinda, alisema kuwa chuo hicho kimekuwa mkombozi kwa watu mbalimbali wanaopita kujiendeleza kielimu.
"Tunawashukuru viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichoshirikiana washirika wake wa vyama vya Ukombozi, kwani kimekuwa mkombozi katika nyanja ya elimu," alisema Mramba.
Mmoja wa Washiriki wa mafunzo hayo Shauri Selenda Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Bagamoyo, amesema kuwa mafunzo hayo yana tija kwani yanalenga kuwajengea uwezo zaidi washiriki kwenye kazi zao.
"Nitumie fursa hii kuwashauri Wakurugenzi wenzangu nchini tukitukie chuo hiki kujiendeleza kielimu, kwani kimejengwa kwa madhumuni hayo," alimalizia Selenda.
Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda akizungumza kwenye ufunguzi wamafunzo ya uongozi kwa viongozi leo Julai 31 kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo maeneo ya ya Kwamfipa Wilayani Kibaha Mkoani Pwani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...