Na. Damian Kunambi, Njombe.
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amesema atawasilisha bungeni maombi ya kuwepo kwa mbegu za ruzuku na hasa mbegu za mahindi ili kuweza kuwapunguzia wakulima gharama za kilimo na kuwafanya waweze kuona faida katika nguvu na uwekezaji wanaoufanya.
Mbunge huyo ametoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Lupande kata ya Mawengi mara baada ya kuwasili kijijini hapo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kupita kijiji kwa kijiji kwa lengo la kutoa mrejesho na kusikiliza changamoto mbalimbali za wananchi ambapo mpaka sasa tayari ametembelea vijiji 45 kati ya 77.
" Lengo la Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ni jema sana kwa wakulima kwani amelenga kuwapandisha hadhi wakulima kwa kufanya kilimo chenye faida na manufaa, ndiyo maana akaleta mbolea za ruzuku hivyo ninaimani suala hili la mbegu za ruzuku pia litafanyiwa kazi". Amesema Kamonga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...