Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewapongeza wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Taasisi ya Benjamin William Mkapa (BMF) na kampuni tanzu Imara Horizon kwa fikra sahihi za uwekezaji wa jengo la Benjamin William Mkapa Health Plaza .
Rais Dk. Mwinyi ambaye pia ni Msarifu wa Taasisi hiyo amesema kwa hatua ya uwekezaji wa jengo hilo ambalo litakuwa linatoa huduma za afya na ofisi kwa mashirika ya afya ni kielelezo kimojawapo cha mafanikio na kutimiza maono ya kumuenzi Hayati Benjamin William Mkapa.
Ameyasema hayo leo katika hafla fupi ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Benjamin William Mkapa Health Plaza lililopo Kawe Jijini, Dar es Salaam.
Aidha, Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendeleza jitihada za kuongeza uwekezaji katika sekta ya Afya hususan katika ujenzi wa miundombinu, ununuzi wa vifaa tiba na upatikanaji wa watumishi wa sekta ya Afya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...