NA VERO IGNATUS,ARUSHA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani amefungua mkutano wa 53 wa Jukwaa la Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-PF)uliofanyika leo Jijini Arusha ukiwa na lengo la kujadili masuala ya kilimo, mikakati kupunguza uhaba wa ajira, sambamba na usalama wa chakula katika ukanda huo
Akizungumza wakati akimkaribisha Mhe.Rais ,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson amesema katika mkutano huo watakuwa wakijadili Maendeleo ya kilimo hasa katika uwekezaji wa Kilimo biashara na usalama wa chakula barani Afrika lengo ni kuhakikisha nchi za SADC inajitosheleza Kwa chakula.
Amesema kwamba mabunge ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC yamekutana kujadili mambo mbalimbali ambapo huu ni Mkutano wa 53 na Tanzania Mara ni nne kukusanya mabunge hayo,''Kauli mbiu kufanya kilimo kuwa cha kisasa ili kukabiliana na uhaba wa chakula na ukosefu wa ajira kwa vijana katika ukanda wa SADC''
Kwa Upande wake Waziri wa Kilimo Husein Bashe amesema kwamba Mkutano huo utajadili suala Zima la mabadiliko ya tabia nchi unaoendana na ugharamiaji wa Kilimo na shughuli za uchumi Kwa mataifa yanayoendelea kuacha kuomba kwenye mataifa ya nje ya bara letu.
Alisema kwamba Sasa ifike wakati Bara la Afrika kujadili namna watakavyoingia kwenye jukwaa la kimataifa kuleta changamoto ya namna ya kupata mitaji badala ya misaada Kwani gharama za mikopo Kwa nchi za bara hili ni kubwa wakati soko ni Moja tofauti na wenzetu wa mataifa ya Ulaya.
"Kujenga Mpango wa kesho iliyobora (BBT) ni Mpango wa miaka nane ambao unachukuwa vijana 1.5 na sio kwamba utacha vijana Kwani Kwa Sasa ni mwaka wa kwanza tunachukuwa Ardhi na mashamba ambapo tumepata fedha Kutoka benki ya Maendeleo Afrika (AFDB) zaidi ya bilion 200 ambazo zimelenga kwenye Mpango huo"
Awali Waziri wa Maliasili na Utalii Mohammed Mchengerwa Amesema kwamba Mkutano huo umefungua fursa za utalii wa mikutano na kama wizara wanajipanga kuhakikisha ukanda huu ambao ndio kitovu Cha utalii unafunguka
Alisema Mikakati ya kukuza utalii wa mikutano ni Moja yake hivyo eneo hilo wanajipanga kuhakikisha wanatengeneza kumbi kubwa zaidi zitakazosaidia uwepo wa mikutano mingi.
Roger Mancienne Rais wa Jukwaa la Wabunge SADC amempongeza Rais wa Jamhruri ya Muungano wa Tanzania kwakupambana kuwa na usawa wa Kijinsia kwa nchi kuwa na Rais Mwanamke kiongozi Spika na baadhi ya wizara kuongozwa na wananwake,kwani hilo ni jambo la kuigwa japo kuwa bado zipo changamoto za kijinsia katika mataifa mengine
Aidha amezitaka nchi za SADC kuwa na uchaguzi huru na wa haki, wabunge kujadili masuala ya serikali, migohoro uongozi , kiuchumi na masuala yenye umuhimu katika pande zotena kuleta tija uelekeo mzuri kwa manufaa ya ukanda huo.
Regina Esparon mwenyekiti wa jukwaa la wanawake ukanda wa SADC amesema bado ipo changamoto ya usawa wa kijinsia ambapo jitihada za ziada zinahitajika ili kuhakikisha kunakuwa na nguvu za kufanya mapinduzi katika usawa wa jinsia kwenye uongozi.
Amesema kuwa takwimu za utafiti African Barometer zinaonyesha ni asilimia 22 pekee ya wanawake ndiyo wanaoshika nafasi za uongozi katika mabaraza ya mawaziri ya nchi za Afrika za Afrika ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia kwani bado wanawake wengi katika jamii za kiafrika hawaruhusiwi kumiliki ardhi wala kuwa viongozi haswa kwenye eneo la kisiasa.
Ametilia mkazo suala la uwezeshwaji wa wanawake katika shughuli za kilimo, huku akisisitiza kuwa ndilo kundi linalofanya kazi kubwa, lakini linakabiliwa na changamoto ya uwezeshaji, hivyo ni vyema kuangalia namna vikwazo hivyo vinatatuliwa ili kuwapa nafasi wanawake wawe na mchango katika sekta ya kilimo katika nchi za SADC.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson wakati akielekea kushiriki na kufungua Mkutano Mkuu wa 53 wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-PF) uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha 03 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akielekea kufungua Mkutano Mkuu wa 53 wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-PF) uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha 03 Julai, 2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...