NA.VERO IGNATUS,ARUSHA
-NI MIONGONI MWA MAKOSA YANAYOVUKA MIPAKA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema serikali imeweza kuokoa kiasi na kuthibiti matumizi ya fedha yasiyostahili Zaidi ya shilingi bilioni 139 kuanzia mwaka wa fedha 2019/20hadi 2021/22 kwa kupitia divisheni ya mahakama kuu inayosikiliza kesi za washtakiwa wa makosa ya rushwa kubwa.
Amesema hayo katika kilele cha maadhimisho ya mapambano dhidi ya rushwa Barani Afrika na Maadhimisho ya utekelezaji wa miaka 20 ya Mkataba wa Umoja wa Afrika wa kuzuia na kupambana na rushwa kwamba viongozi wote hawana budi kuimarisha mapambano na Dunia itambue kuwa Afrika siyo salama kwa wala rushwa
‘’ Nataka niwaelezee kwa kifupi safari ya Tanzania katika utekelezaji wa mkataba huu,sisi Tanzia tulisaini novemba 5,2003 na kuridhia 22februari 2005 na tulianza kuutumia rasmi tarehe 5Agosti 2006 ,leo Tanzania ni miongoni mwa nchi 48 kati ya nchi 55zilizosaini na kuuridhia mkataba huu na tumekuwa tukiadhimisha siku hii tangu mwaka 2018,kufuatia uamuzi wa umoja wa Afrika Julai 2017 ulifanya 11julai kuwa siku ya kupiga vita rushwa’’Alisema Mhe.Samia.
‘’Tanzania ilitunga sheria ya kupambana na rushwa no 11mwaka 2007 ambapo sheria hii ndoiyo iliyoanzisha Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa na kujumuisha pia makosa ya rushwa yanatotajwa katika mkataba wa Umoja wa Mataifa 2003 na nchi ipo katika mchakato wa kufanya mapitio ili iendane na wakati tulionao’’Alisema Rais
Aidha Mhe.Samia amesema moja ya vikwazo barani Afrika ni janga la rushwa vitendo hivyo ni miongoni mwa makosa yanayovuka mpaka,katika mjadala ulioondelea umeonyesha kuwa baadhi ya makundi yanayoongoza kwa rushwa ni Jeshi la Polisi,Wanasiasa,vyuo vya elimu ya juu,Mahakama na wafanyabiashara hivyo ni vyema wakajitathmini na kujirekebisha.
Samia amesema serikali imejiwekeza katika matumizi ya mifumo ya tehama inayosaidia kupunguza mawasiliano ya ana kwa ana katika kutoa huduma kama michakato ya zabuni usajili wa biashara nan amba yam lipa kodi ili kupunguza mianya ya rushwa.
Kwa upande wake Waziri wa nchi Ofisi ya Rais katiba,sheria,utumishi na utawala bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman amesema rushwa inaumiza wanyonge na inaumiza kila mahali hivyo kila mmoja kwa upande wake ashiriki vyema vita dhidi ya rushwa,ambapo wanategemea siku moja Afrika kuwa huru kutoka kwenye janga la rushwa
Suleiman amesema kuwa wanatarajia kuja na mbinu mpya katika mapambano dhidi ya rushwa,kwani Zanzibar imepitisha sheria bora ya mapambano dhidi ya rushwa ,hivyo kupitia maadhimisho hayo Afrika nzima itakuwa na msimamo mmoja katika mapambano dhidi ya vita hii ya rushwa.
Akizungumza mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru CP.Salum Rashid Haamduni amesema kuwa Maadhimisho ya siku ya mapambano dhidi ya rushwa hufanywa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika zilizosaini na kuridhia AUCPCC,ambapo ni sehemu ya utekelezaji wa mkataba huo ambapo madhumuni yake ni kutafakari mapambano dhidi ya rushwa
‘’ Makosa ya dawa za kulevya mara nyingi huchochewa na uwepo wa vitendo vya rushwa’’ alisema Hamduni
Hamduni alifafanua kuwa mara baada ya kelele cha maadhimisho ya kupambana na rushwa Barani Afrika julai 11,2023 siku ya kesho julai 12 kutakuwa na mkutano wa mkubwa wa wa wakuu wa Taasisi za kuzuiz na kupambana na rushwa wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.
''Mkutano huo wa siku moja utahudhuriwa na wa wakuu pamoja na wawakilishi wa Taasisi za kupambana na Rushwa 24 wa nchi wanachama,ambapo kuna washiriki kutoka Zambia,Togo, Congo,Benin,Mali,Sudani Kusini Morocco,Zimbabwe,Bukinafaso,Rwanda,Searalion,Kenya Mourishaz,Djibut,Uganda,Burundi,Ghana,Nigeria,Afrika ya Kusini na mwenyeji Tanzania.
Kwa upande wake waziri wa nchi Ofisi ya Rais menejimenti yautumishi wa Umma na Utawala bora George Simbachawene , amesema uamuzi wa kuadhimishwa kwa siku hiyo ni matokeo ya maazimio ya wakuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika katika mkutano wa 29 uliofanyika julai 3-4,2017 Adis Ababa nchini Ethiopia
''Viongozi waliazimia hili wakirejea tukio muhimu la kihistoria la julai 11,2003 siku ambayo ilipitiswa kuwa na makataba wa Umoja huo wa kuzuia na kupambana na rushwa katika mkutano uliofanyika Maputo nchini Msumbiji''alisema
Katika maadhimisho hayo waliweza kutoa elimu kuhusu madhara ya rushwa katika nyanja mbalimbali,utawala bora utoaji taarifa na malalamiko yatokanayo na rushwa,uhujumu uchumi pamoja na umuhimu wa uchumi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan,akiwa amenyanyua tunzo aliyokabidhiwa Jijini Arusha,kulia kwake ni waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene ,
Baadhi ya Viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Afrika wakiwa katika Maadhimisho ya Kilele cha ya mapambano dhidi ya rushwa Barani Afrika na Maadhimisho ya utekelezaji wa miaka 20 ya Mkataba wa Umoja wa Afrika wa kuzuia na kupambana na rushwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...