KAMPUNI ya ulinzi ya SGA Security imeendelea kulinda hadi yake ya inayotambulika kimataifa katika kutoa huduma za ulinzi hapa nchini.

Kampuni hiyo mwaka huu, ilipata cheti cha ubora chenye nambari ISO 18788 kwa mfumo wake bora katika Usimamizi na uendeshajiwa shughuli za ulinzi hapa nchini.

SGA Security ilipata cheti cha ubira kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 2020, ikiwa ni kampuni ya kwanza nchini kushinda hadhi hiyo muhimu ya kimataifa katika shughuli za kiusalama.

Cheti cha ISO 18788 ni uthibitisho unaothaminiwa sana na taasisi zinazoshughulika na maswala ya usalama kutokana na cheti hicho cha kimataifa ni udhibitisho wa utendaji kazi mzuri, bora na wa viwango vya juu unaofanywa na kampuni za ulinzi. waendeshaji usalama kwani unajumuisha viwango vya juu katika utendakazi vya kampuni iliyoidhinishwa.

Kampuni ya SGA Security ilifanyiwa ukaguzi iliofanywa na kampuni ya ukaguzi wa maswala ya ulinzi ya Intertek Certification Limited ya nchini Uingereza ambayo imeidhinishwa kufanya shughuli hiyo na kampuni ya Huduma za Uidhinishaji ya Uingereza (UKAS).

Uthibitisho wa ubora wa kampuni ya SGA Security umetokana na huduma zake bora inazotoa ikiwemo zile za ulinzi, Usafirishaji wa Pesa, huduma za usalama kwa kutumia mfumo wa kielektroniki, pamoja na huduma za usafirishaji wa bidhaa za wateja kwa njia ya usalama zaidi.

Akizungumza wakati wa hafla ya kupokea cheti cha ISO 18788 kinachodhibitisha ubora wa huduma zinazotolewa na kampuni ya SGA Security, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Bw Eric Sambu, alisisitiza dhamira ya kampuni hiyo ya kufuata sheria na kanuni zote nchini zinazohusiana na huduma za ulinzi hapa nchini.

"Tunaamini kwamba kuzingatia muongozo unaoendana na hadhi ya leseni yetu ya kufanyia kazi ni njia moja wapo ya kufanya kazi kwa weledi kama inavyotarajiwa na wateja wetu, lengo likiwa kutoa huduma zinazoendana na thamani ya fedha zao”, alisema Sambu.

Aliongeza kusema kuwa SGA Security ni mwanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maadili ya Makampuni ya Usalama Binafsi (ICoCA) ambayo inazingatia na kudumisha kanuni za maadili huku ikizingatia haki za binadamu na ufuasi kamili wa sheria.

Tunajivunia mafanikio tunayonaendelea kuyapata kama kampuni bora ya ulinzi ya kibinafsi hapa nchini kupitia huduma tunazotoa huku tukiakisi kazi nzuri zilizofanywa na waasisi wa kampuni yetu ambao ni pamoja aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) hayati Philemon Mgaya na mshirika wake, Edmond van Tongeren.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya SGA Security, Bw Oscar Mgaya, pia alichukua fursa hiyo kuishukuru menejimenti wa kampuni hiyo kwa kuwa makini katika mchakato uliopelekea kudumisha ubora katika kutoa huduma kwa ushirikiano na wadau wengine huku ukizingatia sheria zinazohusiana na maswala ya ulinzi.

“Kwa mfano wa Waasisi wa kampuni yetu ambao wiki hii tunaadhimisha kumbukumbu tangu watutoke, walikusudia na walifanikiwa kujenga mahusiano yenye manufaa na ndiyo maana serikali na vyama vya wafanyakazi vipo karibu na uongozi wa kampuni yetu kila wakati”, alisema Mgaya.

Mgaya aliendelea kusema kuwa kampuni hiyo imeendeela kuimarika katika uendaji shughuli zake kila mara huku ikizingatia sheria na kanuni zote zinazohusiana na maswala ya ulinzi hapa nchini.

"Tunaahidi kuendelea kujenga mazingira mazuri ya kufanya kazi huku tukitumia watumishi wenye weledi na wenye taaluma zinazohitajika katiak kutoa huduma zetu, yote ni katika kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma kama wanavyotarajia”, alisema.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na kamanda wa polisi Mkoa wa kipolisi wa Kindondoni ACP Mtatiro Kitinkwi na Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Makampuni ya Ulinzi Binafsi Tanzania (TUPSE), Charles Basondole.

Viongozi wote hao waliipongeza kam puni ya SGA Security kwa kuwa mfano bora katika tasnia ya ulinzi binafsi.

SGA Security ni moja ya makampuni kongwe ya ulinzi hapa nchini ambayo ilianza kkufanya shughuli zake mwaka 1984.

Kwa ina jumla ya wafanyakazi Watanzania 5,000 wanaofanya shughuli zao kupitia matawi ya kampuni hiyo nchini kote.

Tayari imeshatunukiwa vyeti vingine vitatu vya kimataifa vyenye hadhi ya ISO - 9001, 14001 na 45001.
Mkurugenzi Mtendaji wa SGA, CPA Eric Sambu (kushoto), Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni ACP Mtatiro Kitinkwi (katikati) na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya SGA, Bw. Oscar Mgaya wakionesha cheti cha ubora chenye nambari ISO 18788 ambacho SGA imekuwa ikitukuniwa kwa miaka mitatu sasa ikiwemo mwaka huu. Halfa hiyo ya kuonesha cheti hicho ilifanyika sambamba na kuwaaga wastaafu wa kampuni hiyo na kuwaenzi waanzilishi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...