Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cameroon, Mhe. Felix Mbayu katika Ofisi za Waziri huyo zilizopo Jijini Yaounde nchini Cameroon leo tarehe 21 Julai, 2023.
Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cameroon, Mhe. Felix Mbayu katika Ofisi za Waziri huyo zilizopo Jijini Yaounde nchini Cameroon leo tarehe 21 Julai, 2023.Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia amemshukuru Waziri huyo kwa niaba ya Mawaziri wengine ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Mawaziri ya Umoja wa Afrika (AU) kwa kupitisha jina lake kuwa Mgombea pekee wa Urais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) anayeungwa mkono na AU.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...