Katika kukuza ushirikiano wa Kidipromasia kati ya Japani na Tanzania, Balozi wa Japan hapa nchini Misawa Yasushi ametoa vitabu 61 vyenye machapisho yanayohusu Japani kwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi, watafiti na wasomi wanaopata nafasi ya kutembelea nchi hiyo, kuweza kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa wataalamu wa Japani.

Vitabu hivyo vimetolewa kupitia Mradi wa kukuza tamaduni za kijapani unaosimamiwa na Tokyo Foundation toka mwaka 2008 ukiwa na lengo la kusaidia shughuli za Kitafiti na kukuza uelewa wa wataalum kutoka Japani ili kuchangia maendeleo ya Rasilimali Watu.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda amesema utoaji wa vitabu hivyo ni mwendelezo wa mashirikiano baina ya Chuo cha SUA na Taasisi za Japani yalioadhishwa toka miaka ya 70 ambapo ameleza kuwa vitabu hivyo vitawasaidia wanafunzi na watafiti kuweza kujifunza tamaduni za nchi hiyo.

Kwa upande wake Balozi wa Japan hapa nchini Misawa Yasushi amesema Chuo Kikuu SUA ni chuo cha 4 kujiunga na Mradi huo awali walitoa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dodoma na Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam ambapo mpaka sasa wametoa vitabu 101 nchi nzima.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uzamili, Utafiti, Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri wa Kitaalum Prof. Esron Karimuribo amesema kuna miradi zaidi ya 6 ukwemo Mradi wa Zao la Vanira mkoani Morogoro inaotekelezwa na SUA kwa kushirikiana na vyuo mbalimbali kutoka nchini Japani.

“Katika ushirikiano wetu baina ya SUA na vyuo vya Japani tuna maeneo makubwa ambayo yamesababisha matokeo makubwa, moja ukienda nyanda za juu kusini Mbinga tumeanzisha kilimo kwenye milima ya Matengu kilichosaidia kuzuia mmomonyoko wa ardhi pia kwa Morogoro mafanikiwa ni makubwa ya mazao ya Vanira”. Alisema Prof. Karimuribo.

Hafla ya kukabidhi vitabu ni mwendelezo wa mashirikiano kati Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo na Serikali ya Japani kupitia vyuo mbalimbali vya Japani imefanyika SUA Kampas Kuu ya Edward Moringe Sokoine.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda akipokea vitabu kutoka kwa Balozi wa Japan hapa nchini Misawa Yasushi kwenye hafla ya kukabidhi imefanyika SUA Kampas Kuu ya Edward Moringe Sokoine.
Balozi wa Japan hapa nchini Misawa Yasushi akizungumza  kwenye hafla ya kukabidhi vitabu Kwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) imefanyika SUA Kampas Kuu ya Edward Moringe Sokoine, Julia 27/ 2023.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...