Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg. Hemed Suleiman Abdulla amepongeza hatua ya Viongozi wa Jimbo la Mwanakwerekwe kujenga kituo cha wajasiriamali ili kuwasaidia vijana kuweza kupata ujuzi na kujikimu kimaisha.
Mhe. Hemed ameyasema hayo wakati alipotembelea kituo cha wajasiriamali Jimbo la Mwanakwerekwe ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua uhai wa Chama katika Majimbo yote ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Amesema kuwepo kwa kituo hicho kunaunga mkono dhamira ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwawekea mazingira mazuri wajasiriamali.
Ameeleza kuwa kituo hicho kinasaidia kuwapatia ujuzi vijana wa Jimbo hilo na majimbo mengine na hatimae kuzalisha ajira nyingi zitakazowanufaisha vijana wa Zanzibar.
Akitoa taarifa ya Kituo cha Ujasiriamali Jimbo la Mwanakwerekwe Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu. Said Saleh Said ameeleza kuwa kituo hicho kimeanza rasmi mwaka 2022 kikiwa na lengo la kuwapatia elimu ya Ujasiriamali Vijana ili waweze kujiajiri pamoja na kujikimu kimaisha na kuondokana na mawazo potevu ya kujihusisha na Vikundi viovu.
Amesema tokea kuanzishwa kwake kituo hicho kimezalisha vijana wenye taaluma na uweledi mkubwa kwa kuzalisha bidhaa zilizo bora na zenye viwango pamoja na kuanzisha kitengo cha tehama kwa ajili ya kutoa elimu ya Habari na mawasiliano.
Katika ziara hiyo Mjumbe huyo wa kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amezungumza na wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi na kueleza kuwa Jimbo la Mwanakwerekwe ni miongoni mwa Majimbo yaliyonufaika na miradi mingi ya kimaendeleo ambayo itawanufaisha wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Aidha Mhe. Hemed amewasihi wazazi na walezi kuwasimamia vijana wao ambao wameshafikia umri wa kupata Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi kuhakikisha wanpata itambulisho hivyo pamoja na kujitokeza kwa wingi wakati wa Daftari la kudumu la wapiga kura ili kukipatia ushindi Chama Cha Mapinduzi wakati wa uchaguzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Mwanakwerekwe Ramadhan Fatawi Issa amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuelekeza miradi mingi ya maendeleo katika Jimbo hilo ikiwemo Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Magharibi B, Skuli za Ghorofa, barabara za ndani, Soko la kisasa na ujenzi wa Barabara za juu (FLYOVER) zinazotarajiwa kujengwa mwanzon mwa mwezi huu.
Amesema ni dhahiri Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameamua kwa dhati kuwafikishia huduma bora wananchi wake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ndg. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Mwanakwerekwe katika Kikao kazi wakati wa ziara yake ya kuimarisha Chama katika Jimbo hilo ambayo atatembelea majimbo yote Unguja na PembaKatibu wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Mwanakwerekwe Shaban Rajab Mwinyikombo akisoma taarifa ya Kazi za Chama na Jumuiya zake kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alipofanya ziara ya kukagua uhai wa Chama katika Majimbo yote ya Uchaguzi Zanzibar.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ndg. Hemed Suleiman Abdulla ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa akishona nguo katika Kituo cha ujasiriamali Jimbo la Mwanakwerekwe alipotembelea Kituo hicho katika ziara yake ya kukagua uhai wa Chama Jimboni humo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa Ndg. Hemed Suleiman Abdulla akiwa katika Picha ya pamoja na wanafunzi wa kituo cha ujasiriamili Jimbo la Mwanakwerekwe alipofanya ziara ya kukagua uhai wa Chama katika Jibo hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...