NA WILIUM PAUL, ROMBO.
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga amewataka Wanaume wilayani Rombo mkoa Kilimanjaro kujijengea tabia ya kwenda katika vituo vya afya kucheki afya zao ili kujua kama wanamaambukizi ya virusi vya ukimwi.
Ummy alitoa kauli hiyo jana alipofanya ziara katika wilaya hiyo ambapo alisema kuwa, kwa mujibu wa takwimu zinaonyesha kuwa wakinamama wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kucheki afya zao kuliko wanaume.
“Hapa mmenipa takwimu za watu wanaoishi na virusi vya ukimwi wanawake ni 477 na wanaume ni 159, inaonyesha kuwa wanawake wamekuwa na mwamko wa kujitokeza kwa wingi kupima kuliko wanaume hivyo niwaombe wanaume msiogope kupima na ikitokea mnavirusi vya ukimwi mtaanza kutumia dawa za kufubaza” alisema Naibu Waziri Ummy.
Alisema kuwa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani kwa upendo mkubwa alionao kwa Watanzania amekuwa akitoa fedha nyingi za kugharamia mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi ambapo bajeti ya mwaka wa fedha uliyopita ilikuwa Bilioni 14 lakini mwaka huu w fedha imetengwa bajeti ya Bilioni 25.
Naibu Waziri huyo aliwahakikishia wananchi wa Rombo na Tanzania kwa ujumla kuwa dawa za kufubaza virusi vya ukimwi zitaendelea kutolewa bure kwani Serikali inagharamia.
Aidha Naibu Waziri huyo alisema kuwa, katika wilaya ya Rombo ipo silka ya unyanyapa, unyanyasaji na ubaguzi dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi na kutumia fursa hiyo kukemea jambo hilo na kuwaasa kuacha tabia hiyo kwani inachafua taswira ya Rombo.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Rombo, Kanali Hamisi Maiga alisema kuwa, maambuzi mapya ya virusi vya Ukimwi katika wilaya ya Rombo yamekuwa yakipungua kila mwaka hii ni kutokana na elimu ambayo imekuwa ikiendelea kutolewa katika maeneo mbalimbali ya mikusanyiko ya watu.
“Tumekuwa tukitoa elimu katika maeneo mbalimbali na makundi ya watu kuhusiana na kujikinga dhidi ya ugonjwa huu ili kuepuka kupata maambukizi mapya na hili limeonyesha kuzaa matunda kwani takwimu zimekuwa zikiendelea kushuka kila mwaka” alisema Kanali Maiga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...