Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ambaye pia ni Mbunge wa Mkoa wa Njombe (Viti Maalum), amekabidhi vifaa vya michezo ikiwemo mipira pamoja na mabati 152 katika Shule ya Sekondari Madilu iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe.

Mhe. Chana amekabidhi vifaa hivyo Julai 1, 2023 shuleni hapo ambapo amewasitiza wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii, kuongeza nidhamu pamoja na kuonesha vipaji vyao katika Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuwa ni miongoni mwa sekta zenye fursa ya ajira kwa sasa.

"Masuala ya Utamaduni, Sanaa na Michezo lazima yapewe kipaumbele, kila shule inayosajiliwa lazima kuwe na miundombinu ya michezo ambapo katika shule 56 za michezo zilizotengwa zikiwemo Matola na Makambako za Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa shule zitakazokarabatiwa kwa ajili ya kukuza michezo, amesema Mhe. Chana

Ameongeza kuwa, katika mwaka huu wa fedha wizara itatekeleza Programu ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mtaa kwa Mtaa ambapo amesisitiza jamii kutobadilisha matumizi maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya michezo pamoja na kuyalinda.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mhe. Victoria Mwanziva amewataka wazazi kusimamia wanafunzi wa shule hiyo na nyingine kuhudhuria masomo, pamoja na kushiriki shughuli za maendeleo katika wilaya hiyo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...