Na Nasra Ismaili , Geita
Takribani wanakijiji 6364 wa kijiji cha Inyara kilichopo katika mkoa wa Geita wamenufaika na mradi wa kisima ambacho kimechimbwa na RUWASA mkoani humo ambacho kina uwezo wa kuzalisha maji zaidi ya lita elfu 15 kwa saa ikiwa ni katika kuendelea na mapambo dhidi ya kumaliza tatizo la maji vijijini.
Akitoa taarifa hiyo wakati wa kufungua mradi huo meneja wa RUWASA mkoa wa Geita Injinia Jabir Kayira alisema mkoa wa geita ni miongoni mwa mikoa ambayo inakabiriwa na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji hali iliyopelekea kuathiri upatikanaji wa maji mkoani humo hivyo kuwasukuma kuanzisha miradi mbalimbali ya uchimbaji wa visima ambapo mpaka sasa tayari kuna visima takribani 56 vimeshachimbwa.
Kayira aliongeza kuwa RUWASA ina ahidi kuendelea kutekeleza miradi hii kwa kasi ili wananchi waweze kunufaika na maji yatakayopatikana kwenye visima hivyo na kuwaasa wananchi kutunza miradi hiyo ili ifanye kazi kama ilivyokusudiwa
.“Tunaendelea kuwakumbusha na kuwasisitiza wananchi tuendelee kutunza na kuhifadhi vyanzo vya maji na ndio maana tunaina leo tumechimba kisima kirefu ambacho kina urefu wa zaidi ya mita 100 lakini pia kinatoa maji zaidi ya lita elfu 15 maji haya ni mengi tukiyatunza yanaweza kuhudumia kijiji hiki kwa mda mrefu sana” Alisema Kayira.
Nae meneja wa RUWASA wilaya ya Geita Sunday Batakanwa ambaye pia ndiye alisimamia mradi huo alisema kuwa mradi huo umefanikiwa kwa asilimia 100 kwani kisima kinatoa maji lita 380000 kwa siku ikilinganisha na mahitaji ambayo ni laki 175000 .
“ tumejenga vituo 8 lakini pia tumejenga tank la lita 225000 pia tumesambaza mabomba kilometa 13.8 na huduma hii imewafikia wananchi kwa asilimia 100.”Alisema Batakanwa.
Kwa upande wao wananchi wameishukuru RUWASA kwa kuwaletea kisima hicho kwani kabla ya kisima hicho wamekuwa wakichota maji katika bwawa ambalo lilikuwa na maji yasiyo salama kwani walilitumia pamoja na mifugo yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...