Wazairi Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda ameitaka Serikali kudhibiti uzalishaji holela wa Vifaranga vya Samaki ili kuwasaidia wafugaji kupata mbegu bora ya Vifaranga vya Samaki
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ameyasema hayo mkoani Morogoro kwenye Maonyesho ya wakulima Nanenane Kanda ya Mashriki wakati alipotembelea Banda la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
Amesema kuna haja ya kuwepo kwa Mamlaka itakayo kuwa inasimamia ubora wa Vifaranga vya Samaki ili mfugaji anapopata Vifaranga visivyokuwa na ubora kuwe na Sehemu ya Kutoa Taarifa na kupata msaada.
Aidha, Pinda amekipongeza Chuo cha SUA kwa kuwajali wakulima na wafugaji kwa kuja na teknolojia mpya Katika maonesho hayo zitakazowasaidia kuongeza ujuzi na kuzalisha tija.
Awali akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Afisa Mafunzo Shamba la Mafunzo ya Mfano kutoka SUA Bi.Stella Genge amesema SUA kupitia Ndaki ya Kilimo, Idara ya Sayansi ya Wanyama, Viumbe Maji na Malisho imejikita katika kuzalisha vifaranga vya samaki na kutoa elimu bora jinsi ya kutunza samaki, pia inazalisha chakula cha samaki majani aina ya azola ambayo ni mojawapo ya chakula kizuri cha Samaki na Mifugo mingine kama vile kuku, ng’ombe na wanyama wengine wafugwao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...