Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotions Alex Msama amesema watanzania wanapaswa kumheshimu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani Mwenyezi Mungu ametupa mtu ambaye anaendelea kufanya kazi vizuri kwa manufaa ya Taifa la Tanzania.

Pia amesema anakerwa na watu ambao wamekuwa wakitoa lugha za kashfa , kejeli na dharau katika mitandao ya kijamii dhidi ya Rais Samia huku akitumia nafasi hiyo kuziomba Mamlaka kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu hao.

Msama ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ametumia nafasi hiyo kuelezea namna anavyochukizwa na baadhi ya watu wanaofanya dhihaka dhidi ya Rais Samia.

Hivyo amewataka watu hao kuacha mara moja kumkashifu Rais Dk.Samia huku akielezea kwa kina jinsi Rais anavyofanya kazi kubwa na nzuri ya kulitumikia Taifa sambamba,kuendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki ya uwekezaji huku hali hiyo ikichagiza ukuaji wa uchumi wa nchi.

"Chini ya Rais wetu Dkt.Samia uchumi wetu unaendelea kuimarika. Rais ni Mama wa familia kama alivyo mzazi wako, tuache kutoa kauli ambazo sio rafiki, zinazomdhihaki , " amesisitiza Msama.

Awali wakati anazungumza Msama pia ameipongeza Kamati Kuu (NEC ) ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kwa kutoa elimu inayoelezea umuhimu wa uwekezaji nchini.

Amesema kutokana na elimu inayoendelea kutolewa na CCM kupitia viongozi wake kuhusu uwekezaji wananchi wengi wameanza kuwa na uwelewa kuhusu uwekezaji.

Msama amesema kuna watu ambao kazi yao imekuwa ni kupotosha ukweli kuhusu uwekezaji, lakini anaipongeza CCM na viongozi wa Serikali kueleza ukweli ambao umesaidia wengi kuelewa ukweli na nini kinachoendelea.

MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotions Alex Msama alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 12,2023 jijini Dar es salaam.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...