*Azungumzia utekelezaji miradi ya kimkakati, uboreshaji huduma za afya

* Awataka waache kufuata mkumbo kumtukana Rais,agusia suala la udini

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam ameelezea kwa kina mambo makubwa ambayo.yamefanywa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika kipindi kifupi huku akiendelea kujenga mifumo mizuri ya kiuchumi ambayo ndio silaya ya kila jambo katika taifa hili.

Amesisitiza pia Rais Samia ameendelea kuendeleza miradi yote aliyoikuta waliyokuwa wanafanya na mtangulizi wake na kwamba miradi hiyo ni mikubwa na ni mingi leo katika nchi zote za ukanda wa SADC nchi.

Akizungumza na wananchi wa Mbagala jijini Dar es Salaam baada ya kukagua miradi ya maendeleo na kufungua soko jipya la Zakhiem , Chalamila ametumia nafasi hiyo kuelezea miradi inayoendelea kutelekezwa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia.

"Sijaja kufanya siasa hebu niwaeleze kidogo pale Muhimbili juzi wamekuja marais kutoka Bara la Afrika tumewapokea hapa uwanja wa ndege.Tanzania hii Mungu amewapa neema kubwa.

" Naomba nieleze aliyoyafanya Rais Samia katika muda mfupi, jambo la kwanza na hii ilikuwa ukipatikana na uvimbe kichwani ilikuwa mpaka uende India kwa hiyo Rais Samia amefunga mitambo pale muhimbili mashine moja inauzwa zaidi ya bilioni 35 .

"Huu ubongo mnaouna upo hapa juu na kwa chini ilikuwa kama kuna uvimbe kwenye ubongo kwa chini ilikuwa lazima wapasue kichwa wautoe ubongo waondoe uvimbe warudishe ubongo halafu washone kichwa, " amesema Chalamila.

Amefafanua sasa hivi uvimbie unaondolewa kwa kuingiza vifaa vichache kichwani kwenda kulainisha kwenye uvimbe halafu unaondoka bila kwenda India.

Pia amesema zamani ilikuwa mtu akipata kiharusi ilikuwa inakawia kupona lakini hivi sasa Rais Dk.Samia ameweka kifaa kimoja kikubwa chenye thamani ya mabilioni ya fedha ambacho kinafanya kazi ya uyeshushaji wa mifumo ya damu ili kuruhusu mgonjwa huyo kupata nafuu haraka na kuendelea na shughuli zake

"Kwa bara la Afrika kinapatikana katika nchi tatu Tanzania , Afrika Kusini pamoja nadhani na Misri.Lakini mlikuwa mnaona wagonjwa saratani zamani ilikuwa ili utibiwe saratani na mionzi ile mionzo unayoiona inaagizwa Afrika Kusini na inatakiwa inaposafirishwa isizidi saa mawili na nusu iwe imeshamfikia mgonjwa.

" Leo hii Rais Samia pale Ocean Road amenunua kifaa cha zaidi ya Sh.bilioni 40 ambacho kinazalisha ile dawa ya mionzi na kinakutibu pale tu ambapo kwenye dalili za kansa kwa hiyo leo yale mambo ya kunyonyoka nywele hayapo tena kwasababu rais amefunga mtambo mkubwa pale."

Ameongeza pia zamani ilikuwa unatoka hapa kwenda kupandikiza mimba Afrika Kusini lakini Rais Samia amenunua vifaa maalum ambavyo vipo pale Muhimbili, ukienda pale unapandikiza mimba yako na unazaa kama wanavyozaa wengine.

Amesema uwepo wa huduma hiyo umepunguza watu kwenda Ulaya na Afrika Kusini kwani huduma hiyo inapatikana Muhimbili.Hayo maajabu yako hapa hapa Tanzania yako hapa Muhimbili chini ya utawala wa Rais Samia."

Pamoja na hayo amesema katika ziara yake wilayani Temeke amekwenda kuiangalia barabara barabara ya Nzasa mpaka Buza ambayo imejengwa kwa Sh.bilioni 16.4 na hiyo barabara kwa asiyejua imejengwa ndani ya miaka miwili tangu kuingia madarakani kwa Rais Samia.

Amesema fedha hizo zimefadhiliwa na mradi wa Benki ya Dunia lakini mtafutaji wa fedha hizo ni Rais Samia Suluhu Hassan."Lile daraja nimeliona pale barabara ziko nyingi zipo karibu barabara za aina tatu zote zinatofautina bei zake ...

"Na ile barabara ndio imetengenezwa kwa bei ya juu na inataa 161 , taa moja ni zaidi ya Sh.milioni tatu , ina makaravati makubwa yenye masikio sita na kuna daraja kubwa moja maana yake ni kwamba barabara hiyo ni makofi mengi kwa Rais wetu ameendelea kuiunganisha mbagara yetu.

"Lakini kwenye miradi ya barabara mmeona pia hii barabara iendayo kwa kasi ambayo leo vijana wetu wanatumia kuuza bidhaa zao pale barabarani.Naomba leo nitangaze tunawapenda sana lakini sio kuuzia pale barabarani, leo basi likipotea pale mtaanza kusema mkuu wa mkoa mzembe...

" Mkuu wa wilaya mzembe msiende kupanga barabara ile sio barabara ya wafanyabiashara holela ni barabara ya mabasi yaendayo kwa kasi hapa Mbagala.Hii barabara mnayoiona ni awamu ya pili ya ujenzi ambayo mzunguko wake wote unahitaji mabasi 775 ya mwendo kasi na hii barabara imetumia si chini ya Sh.bilioni 217."amesema.

Pia ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wasiingie wenye mikumbo kuna mtu anajiuliza tu kwanini Samia ni Rais."Anakwenda kumtukana Rais Samia na wewe unajingiza ukidhani kwanini Rais Samia kumbe mwingine anahangaika kwanini Rais Samia ni Rais.

"Aliyeamua Rais Samia kuwa Rais ni Mungu wa Mbinguni ambaye jina lake litabaki kuwa hivyo hivyo na wewe subiri wakati wako utafika.Wakati wote marais huingia darakani kwa njia ambayo Mungu anataka.

" Kwa hiyo msiijingize kwenye mikumbo hiyo ambayo ni ya watu wachache walafi wa madaraka ,na watu wengine wanaotaka kujificha kwenye migongo ya dini kuhatarisha amani ya taifa letu kuona kama vile ni vita kumbe ukristo na usilamu ni urafiki wa kudumu.Mungu tunayemuabudu ni mmoja, "amesema Chalamila.

Ameongeza ameona pia aelezee propaganda za baadhi ya watu ambao wanasambaza uongo Rais kauza bandari, rais kauza bandari.

" Wapo wanasema Chalamila haya mambo ya bandari waachie wenyewe siwezi kukuachia kwa ambaye hujaelewa ukweli, bandari ya Dar es Salaam iko Dar es Salaam na Mkuu wa mkoa ni mimi na kama wewe unataka kuwa mkuu wa mkoa huu subiri muda wako utafiki, bandari ya Dar es Salaam na sera za taifa letu zitaendelea."


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...