Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amechukua hatua ya kufanya mabadiliko ya Uongozi Sehemu ya Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA).

Katika mabadiliko kuisuka mpya menejimenti hiyo iliopo chini ya ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) amentangaza rasmi Mhandisi Mashaka Sitta kuwa Meneja wa DDCA huku akimuweka pembeni Eng. Simon Ngonyani aliekua katika nafasi hiyo.

Waziri Aweso akizungumza na Watumishi wa DDCA ameeleza bayana kuwa harudhishwi na kazi inayofanyika hususani Wizara katika eneo hili muhimu ikiwa imepokea Mitambo mipya ya Uchimbaji Visima na Mabwawa hivo anaamini inahitajika kufanyika maboresho na mabadiliko yatakoyoongeza tija na nguvu mpya ya kufanya kazi.

Aidha, Waziri Aweso ameeleza kuwa mabadiliko haya yanalenga kuongeza ufanisi na usimamizi na kuhimiza uongozi mpya kufanyia kazi mapungufu yote wakati mchakato wa kuifanya DDCA kuwa Wakala ikiendelea.

Katika hatua nyingine naye N/Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Eng Cyprian Luhemeja amesema kuwa maagizo yote aliotoa Waziri wa Maji juu ya dhamira ya kuimarisha utendaji kazi katika eneo hili la uchimbaji visima na ujenzi wa mabwawa yatasimamiwa ipasavyo ili malengo na dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan yaweze kutimia.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...