Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi pamoja na wadau wengine kushiriki kwenye mbio fupi zilizoambatana na matembezi ya hiyari (Wogging) zilizoandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya Zanzibar na Shirika la Kimataifa la Amref Afika, tawi la Tanzania zikilenga kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga Zanzibar.

Kupitia tukio hilo ambalo ni sehemu ya kampeni ya ‘Uzazi na Maisha’ benki hiyo pia ilitoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Tshs Milioni 200 vitakavyotumika kwenye hospitali mbalimbali za Zanzibar ili kuboresha huduma ya afya visiwani humo.

Akizungumza mara baada ya kushiriki matembezi hayo yaliyoanzia eneo la Kiembe Samaki kwa Butros Wilaya ya Magharibi B na kumalizikia viwanja vya Maisara, Zanzibar mwishoni mwa wiki, Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wateja wa serikali Benki ya NBC Linley Kapya alisema mbali na mazoezi ya viungo, ushiriki wa benki hiyo ulilenga kuunga mkono jitihada za Serikali za kupunguza na kuepusha vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga ambapo bado kiwango cha changamoto hiyo kipo juu.

‘’Kama ambavyo amebainisha Rais Dk. Mwinyi kwamba takwimu zinaonesha kuna vifo vya kina mama 134 kati ya vizazi hai 100,000 kwa mwaka na vifo 28 vya watoto wachanga kati ya vizazi hai 1,000 kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2017. Hali hiyo husababishwa na changamoto za huduma duni za mama na mtoto katika hospitali na vituo vya afya zikiwemo uhaba wa wahudumu na tatizo la kukosekana kwa dawa.’’

‘’NBC tukiwa wadau tunaosapoti sekta zote ikiwemo michezo na afya tukaona ni vema kwetu tukiwa sehemu ya jitihada hizi muhimu,’’ alisema.

Kwa mujibu wa Bw Kapya mbali na michezo, Benki hiyo imekuwa mdau mkubwa wa Afya visiwani humo ambapo imekuwa ikitoa huduma za vipimo bure kwa wamama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano kupitia program yake ya Mobile Clinics kwa kushirikia na Wizara ya Afya ya Zanzibar.

Akizungumza kwenye tukio hilo pamoja na kuzungumzia umuhimu wa mazoezi kiafya sambamba na kuwapongeza washiriki wa wogging hiyo, Dk. Mwinyi, alieleza matumaini yake kupitia kampeni hiyo, kwamba Serikali itaongeza vifaa tiba kwa vituo vya afya 28, sawa na asilimia 40.5 ya vituo vyote 69 vinavyotoa huduma za mama na mtoto Zanzibar.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Zanzibar Hassan Hafidh alisema lengo la kuanzishwa kwa kampeni ya “Uzazi ni Maisha” inayohusisha michezo ni kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto nchini.

Naye, Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Amref Afika Tanzania, Dk. Florence Temu pamoja na kuwashukuru wadau mbalimbali walioshiriki kwenye kampeni hiyo pamoja na wanamichezo walioshiriki wogging hiyo, alisema lengo la kuanzishwa kampeni hiyo ya “Uzazi ni maisha ni kukusanya shilingi Bilioni moja kwajili ya kununuliwa vifaa tiba vya hospitali na vituo vya afya 69 vinavyotoa huduma za mama na mtoto, Zanzibar.

‘’Tukiwa kwenye mwaka wa pili wa kampeni hii, Shirika la Amref tayari tumefanikiwa kukusanya milioni 557 na tumepokea ahadi za shilingi milioni 883 ambayo itafikisha lengo la kampeni hii kufikia 2024.’’ Alibainisha.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (wa tatu kushoto) akikabidhi chetu cha shukrani na utambuzi kwa Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wateja wa serikali Benki ya NBC Linley Kapya (wa pili kulia) kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha kampeni ya ‘Uzazi na Maisha’ iliyoambatana na mbio fupi zilizoambatana na matembezi ya hiyari (Wogging) zilizofanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki. Benki hiyo ilitoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Tshs Milioni 200 kufanikisha kampeni hiyo. Wengine ni pamoja na Naibu Waziri wa Afya, Zanzibar Hassan Hafidh (kushoto), Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Amref Afika Tanzania, Dk. Florence Temu (Kulia)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiwa tayari kuongoza washiriki wa mbio fupi zilizo ambatana na matembezi ya hiyari (Wogging) zilizofanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya kufanikisha kampeni ya ‘Uzazi na Maisha’ iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya Zanzibar na Shirika la Kimataifa la Amref Afika, tawi la Tanzania zikilenga kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga Zanzibar.Pamoja nae pia wapo Naibu Waziri wa Afya, Zanzibar Hassan Hafidh (kushoto kwa Rais Mwinyi), Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (kulia kwa Rais Mwinyi) na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Amref Afika Tanzania, Dk. Florence Temu (Kushoto kwa Naibu Hafidh )


Matembezi hayo yalianzia eneo la Kiembe Samaki kwa Butros Wilaya ya Magharibi B na kumalizikia viwanja vya Maisara, Zanzibar.

Maofisa wa Benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wateja wa serikali wa benki hiyo Linley Kapya (kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Amref Afika Tanzania, Dk. Florence Temu (wa pili kushoto) mara baada ya kukabidhiwa chetu cha shukrani na utambuzi wa mchango wa benki hiyo katika kufanikisha kampeni ya ‘Uzazi na Maisha’ iliyoambatana na mbio fupi zilizoambatana na matembezi ya hiyari (Wogging) zilizofanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki. Benki hiyo ilitoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Tshs Milioni 200 kufanikisha kampeni hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...