MKUU wa Wilaya ya Kilombero, Danstan Kyobya na Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi wamefika katika Kata ya Ching'anda na Chita na kumaliza changamoto ya mgogoro wa Wafugaji na Wakulima uliokua umedumu kwa muda mrefu pamoja na kueleza hatua za kimaendeleo ambazo serikali imezifanya kwenye jimbo hilo.
Viongozi hao walifika na kusikiliza changamoto zilizokua zikiwakabili wananchi hao ambapo DC, Kyobya alitoa maelekezo kwa Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kilombero kuwashikilia Wafugaji wawili Orandi Makenzi na Richard Maveregachu kwa ajili ya mahojiano baada ya wananchi wengi kulalamika kuwa wamekua wamekua wakifanya malisho kwa mifugo yao kwenye mashamba yao.
" Serikali ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan inajali ustawi wa wananchi wake, hatupo tayari kuona kundi fulani la watu linalalamikiwa, tunataka watu wote wafanya kazi kwa kufuata sheria, kanunia na taratibu zilizowekwa bila kuathiri kundi lingine," DC Kyobya.
Natoa maelekezo kwa OCD kuwahoji hawa wafugaji wawili ambao wamelalamikiwa kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima na kuathiri mazao yao, hatua za kisheria zichukuliwe itakapobainika kwamba tuhuma hizo ni za kweli," Amesema DC Kyobya.
Kwa upande wake Mbunge Kunambi amemshukuru DC Kyobya kwa kufika katika kata hiyo na kutatua mgogoro huo huku ambapo pia alitumia mkutano huo kueleza mambo makubwa ambayo Rais Dkt Samia ameyafanya katika Jimbo la Mlimba katika sekta mbalimbali za elimu, afya na miundombinu.
" Kipekee kabisa nimshukuru Rais Dkt Samia, ndani ya muda mfupi ametenda mambo makubwa katika Jimbo letu, kwenye sekta ya elimu tayari ametupatia Sh Bilioni 3.5 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Veta ili kutoa elimu na ujuzi wa fani mbalimbali kwa vijana wetu.
Kwenye sekta ya afya Rais Dkt Samia alitupatia Sh Bilioni 1.5 kwa ajili ya Hospitali yetu ya Wilaya ambapo tayari imeanza kufanya kazi kwa kupokea wagonjwa wa nje (OPD) pamoja na huduma za X-ray hii maana yake sasa wananchi wa Mlimba hatutotembea umbali mrefu hadi Ifakara kufuata matibabu kama ilivyokua mwanzo, niwaombe tuendelee kumuunga mkono Rais wetu kwa mambo makubwa anayotufanyia," Mbunge Kunambi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...