MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amewaonya viongozi wa Serikali za vijiji dhidi ya tabia iliojikita kwa baada yao ya kutengeneza migogoro hasa ya ardhi kama sehemu ya kujipatia kipato.

Amesema amebaini maeneo mengi yenye migogoro imetengenezwa na baadhi ya viongozi hao kwa maslahi binafsi hali ambayo inapelekea wananchi kutoiamini serikali yao

Mgeni ameyasema hayo katika mwendelezo wa ziara zake za kusikiliza kero za wananchi ambapo alipofika Kata ya Makanya pamoja na mambo mengine amezungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.

Akihutubia wananchi hao amesema viongozi hao wajue kuwa wana dhamana ya kuhakikisha wanamsaidia Rais Dk.Samiha Suluhu Hassani kutatua kero zinazowakabili wananchi na si kuwa chanzo cha kero na migogoro kwa wananchi .

"Migogoro ya ardhi ambayo wananchi wanailalamikia kwenye kata hii kwa kiwango kikubwa imesababishwa na baadhi viongozi wasio waadilifu kwa kuuza ardhi kiholela na kinyemela huku wananchi wakiendelea kudanganywa kuwa maeneo hayo yamevamiwa na wageni .

" Serikali haiwezi kuvumilia kuwa na viongozi wa namna hiyo ,kama hawawezi kubadilika wakae pembeni kabla hawajaondolewa, "amesema




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...