NA MWANDISHI WETU, TEMEKE
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Mobhare Matinyi, ameungana na
viongozi kadhaa kuhudhuria hafla ya ufungaji ndoa 70 iliyofanyika katika ukumbi
wa Taasisi ya Al Hikma ya Chang'ombe wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mhe. Matinyi ambaye alikuwa alikuwa akimwakilisha
Mkuu wa Mkoa pia alitangaza kumpatia bwana harusi mmoja mlemavu wa miguu, Ally
Kundi, sh. 200,000/- kila mwezi kwa mwaka mzima zikiwa ni za mafuta ya Bajaj
aliyozawadiwa kwa kushtukizwa na Taasisi ya Al Hikma iliyoandaa hafla hiyo.
Taasisi hiyo inayoongozwa na Sheikh Nurdìn
Kishki ilimzawadia Bajaj hiyo Kundi, maarufu zaidi kwa jina la Babu Ally, ili
kumkomboa kiuchumi. Bajaj hiyo ina thamani ya shilingi milioni 9.8.
Awali mara tu baada ya kuipokea zawadi
hiyo huku akitokwa machozi ya furaha, alishangaa tena kusikia viongozi wanne
waliohudhuria hafla hiyo akiwemo Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omar
Kumbilamoto, wakimpatia shilingi milioni mbili za gharama ya mafuta ya kuanzia
biashara yake.
Babu Ally ambaye ni mkazi wa Mwembe Yanga
wilayani Temeke, alikuwa akiendesha Bajaj jijini Dar es Salaam kwa kupeleka
hesabu za jioni kila siku.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na waumini wa
kiislamu zaidi ya 500 wakiongozwa na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar
Zuberi, huku mgeni rasmi akiwa Naibu Spika wa Bunge la Muungano, Mhe. Hassan
Zungu.
Mbali ya kutoa salamu za serikali, Mhe.
Matinyi pia alikabidhi zawadi kwa wadhamini watatu wa shughuli hiyo
iliyofuatiwa na chskyla cha mchana.
Kwa mujibu wa Sheikh Kishki, hii ni mara
ya kwanza kwa ndoa 70 katika dini ya kiislamu kufungwa hapa nchini kwa pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...